Na Mwandishi Wetu, Bagamoyo

VIKUNDI 60 vya burudani kutoka ndani na nje ya Tanzania, vinatarajiwa kushiriki tamasha la 32 la Sanaa linaloandaliwa na Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA), mkoani Pwani, litakaloanza kuanzia Septemba 23 hadi Septemba 28 katika chuo hicho.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kitengo cha Tamasha na Maonesho wa chuo hicho, Abraham Bafadhili ‘Bura,’ alisema, maandalizi yamekamilika ambako wageni kutoka nje ya nchi, wamethitisha ushiriki wao.

“Safari hii, jumla ya vikundi vya sanaa 60, vitashiriki kwenye tamasha la Sanaa la 32, hivyo wananchi wa Bagamoyo na vitongoji vyake wanakaribishwa kujionea shangwe hizo,” alisema Bura.

Alisema, vikundi 40 kati ya 60, ni kutoka Tanzania na vingine ni kutoka nje ya nchi vikiwemo vilivyowahi kushiriki tamasha hilo na vipya ambavyo itakuwa ni mara ya kwanza kuja.

Alivitaja vikundi vya Tanzania kuwa ni Ngome International Magic Show – JWTZ, Splendid Theatre, Kigamboni Community Centre, Malezi Youth Theatre na Jivunie Tanzania Sanaa.

Vingine ni Mapoloni Culture Centre, Albino Revolutionary, Cocodo African Music, Imani Theatre, Safi Theatre, Imara Boma, Bagamoyo House of Talents, Bwagamoyo Africulture, Godykaozya & Tongwa Band na Mtoto Mchoraji.
Vimo pia Shada Acrobatics, Bagamoyo Players, Bayoice, Jikhoman & Afrika Sana Band, Vitalis Maembe & The Spirit Band na Bagamoyo Dance Company.

Aidha, kuna vikundi vya Makini Organization (Arusha), Tumaini Group (Manyara), Kimanzichana Vijana Group (Mkuranga), Utandawazi Theatre Group (Matwi Gha Chalo), kutoka visiwa vya Ukerewe, Hiari ya Moyo (Dodoma), Moshi Police Academy (Moshi), CBM Acrobatic Group, Man Kifimbo Band na Midundo ya Sanaa.

Pia kuna vikundi kutoka Ethiopia, Kenya, Norway, Uganda, Rwanda na Ujerumani.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: