Katika kusheherekea miaka mitatu ya utendaji kazi wake ndani ya ulingo wa matangazo ya digitali Tanzania, kampuni ya Star Media Tanzania imelenga kuongeza vipindi na chaneli zaidi ili wateja wake waendelee kufaidi huduma kulingana na thamani ya fedha zao.
Akizungumza katika sherehe za maadhimisho hayo, afisa habari wa Star Media Tanzania, Erick Cyprian alisema “Star Media imeshawapa thamthilia za kuvutia kama ‘Assinator Jing Ke’ na itaendelea kuleta mfululizo wa thamthilia pendwa ya Kichina ya ‘A scheme of beauty’ ambayo itakuwa na maandishi katika lugha ya Kiswahili ili kuwafanya watanzania wengi waifurahie, maana ina simulizi nzuri na uigizaji wa kuvutia’’ aliongeza bwana Cyprian.
Kwa wale wapenda soka, StarTimes itakuwa ikirusha matangazo ya moja kwa moja ya mechi za soka kwa msimu mpya wa ligi ya Ufaransa na UEFA. Matangazo hayo yatakuwa yakirushwa katika chaneli ya ‘STV Kung fu’ na nyinginezo.
StarTimes inajivunia kuwa kampuni pekee, kupata kibali cha kurusha matangazo ya chaneli ya NBA TV kwenye nchi za Afrika. Kwa maana hiyo wapenzi wa kikapu wajiandae kufurahia matangazo ya moja kwa moja ya mechi kubwa kwa msimu mzima.
Zaidi ya hayo, katika kuwathamini na kuwajali wateja wake, StarTimes ikiwa inasherekea miaka mitatu ya kibiashara nchini, inawapatia ofa wateja wake wote. Mteja atakaye lipia kwa miezi miwili kwa mara moja atapata bonasi ya wiki mbili bure na atakaye lipia miezi mitatu kwa mkupuo atapata bonusi ya wiki nne kwenye kifushi chochote.
“Tunawashukuru wateja wetu zaidi ya laki sita kwa kutuunga mkono na tunawahakikishia kuwapatia bidhaaa na huduma bora zaidi kadri iwezekanavyo.
Kwa sasa tunatoa huduma katika mikoa tisa ambayo ni Dar es salaam, Mwanza, Arusha, Dodoma, Tanga, Moshi, Mbeya, Morogoro na Zanzibar.Tuna mpango wa kupanua zaidi wigo wa huduma zetu kwa mwaka huu katika maeneo takriban sita ambayo ni Bukoba, Musoma, Kahama, Tabora, Singida na Iringa. Hii itafanya uwekezaji wetu kufikia jumla ya dola za kimarekani 265,000,000” alisema Jack Zhoujun, Mkurugenzi Mkuu Msaidizi wa StarMedia Tanzania.
Mbona mnatusahau mkoa wa Kilimanjaro?
ReplyDeleteMbona mnatusahau mkoa wa Kilimanjaro?
ReplyDelete