Kauli mbiu kwenye t-shirt
Maandamano yakitokea uwanja wa mpira wa miguu wa Nyamagana kuelekea Sekou Toure Hospitali.
 Waandamanaji wakielekea Sekou Toure.
Ujumbe lazima umfikie kila mkazi wa jiji la Mwanza.
Mkurugenzi Mkazi wa CDC Dr Michelle Roland na Mkurugenzi Mtendaji wa CSSC Bw Peter Maduki wakiteta jambo wakati wa uzinduzi huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa CSSC Bw. Peter Maduki akitoa salamu na taarifa za mradi wa ART unaotekeleza mpango wa kuwarejesha kwenye matibabu endelevu watu wanaoishi na VVU walioacha wakati wa uzinduzi huo.
Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo, akizindua mpango huu kwa kuliza king'ora kuashiria kuwa mpango huo umezinduliwa rasmi
---
Na Rachel Mkundai - CSSC 

Tume ya Kikristo ya Huduma za jamii (Christian Social Services Commission) CSSC, imezindua mpango maalum wa kuwarudisha wanaoishi na Virusi Vya UKIMWI katika huduma endelevu za matibabu ya VVU katika jiji la Mwanza.

Mpango huo unajulikana kama "Back To Care Initiative" umezinduliwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo katika viwanja vya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou Toure.

Uzinduzi huo umehudhuriwa pia na Mkurugenzi Mkazi wa Centres for Disease Control & Prevention (CDC) Dr Michelle Roland unalenga kurejesha zaidi ya wanaoishi na VVU 8,000 ambao wameacha matibabu kwa sababu mbalimbali kama vile kujisikia vizuri, kunyimwa ruhusa ntoka kwa waajiri wao, kukosa gharama za usafiri n.k. Aidha wanoacha matibabu ni pamoja na watoto wapatao 1600 sawa na asilimia 18 wenye umri chini ya miaka 15.

Madhara yanayotokana na kuacha huduma hizi ni pamoja na kuzorota afya za waVVU na kushindwa kufanya shughuli zao za maendeleo

Mpango huu ambao utajumuisha wilaya za Nyamagana, Magu na Geita, utasaidia kuwawezesha watu waVVU kurejea kwenye huduma endelevu na kauli mbiu ni TIBA NI HAKI YAKO... RUDI KWENYE TIBA LEO!
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: