Afisa Biashara Mkuu wa Zantel, Sajid Khan akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kuzindua ushirikiano baina ya kampuni yake na United Against Malaria. Anayetazama kushoto ni Balozi wa Malaria Tanzania, Leodger Tenga, ambaye pia ni Rais wa Chama cha Mpira Tanzania, na kushoto ni Furaha Kabuye, Meneja wa Mradi wa Malaria.

Balozi wa Malaria Tanzania Leodger Tenga, ambaye pia ni Rais wa Chama cha Mpira Tanzania (TFF) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa ushirikiano baina ya kampuni ya Zantel na United Against Malaria. Kulia kwake ni Sajid Khan, Afisa Biashara Mkuu wa Zantel.
---
Kampuni ya simu za mikononi ya Zantel leo imezindua ushirikiano baina yake na United Against Malaria, ushirikiano wenye lengo la kuongeza nguvu kwenye mapambano dhidi ya ugonjwa hatari wa Malaria.

Ushirikano huu utajumuisha maeneo manne, ambayo ni ushawishi, uenezi na elimu kuhusu Malaria kupitia vipeperushi, semina pamoja na matangazo.

Sehemu nyingine ya ushirikiano huo muhimu itakuwa ni pamoja na kampuni ya Zantel kuandaa mafunzo ya kupambana na Malaria, pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Zantel kuzungumza kuhusu Malaria kwenye mikutano mbalimbali.

Akizungumza wakati wa sherehe za kuzindua ushirikiano huo, Afsa Biashara Mkuu wa Zantel, Sajid Khan, alisema kwa ushirikiano huo kampuni ya Zantel inatarajia kupunguza vifo vitokanavyo na ugonjwa hatari wa Malaria.

“Afya ya wananchi ni muhimu sana kwa kampuni ya Zantel, na kwa ushirikiano huu kampuni yetu inaamini itasaidia kupunguza kama sio kuondoa kabisa vifo vinavyotokana na ugonjwa wa Malaria’’ alisema Khan.

Malaria ni mojawapo ya magonjwa yanayosababisha vifo vingi hapa nchini, ikikadiriwa kufikia 60,000 kwa mwaka huku zaidi ya asilimia 80 ikiwa ni watoto walio chini ya miaka 5.

Kampuni ya Zantel pia itatumia maeneo yake mengine inayodhamini kama Epiq Bongo Star Search na Epiq Open Mic kufikisha ujumbe kwa wananchi wengi zaidi.

‘Hatua kubwa imepigwa kwenye mapambano dhidi ya Malaria, na sisi kama Zantel tunafuraha kushiriki kwenye kueneza ujumbe wa mapambano dhidi ya ugonjwa huu hasa kwa kutumia rasirimali zetu’’ alisisitiza Khan.

Naye balozi wa Malaria Tanzania, Leodeger Tenga, ambaye pia ni Rais wa shirikisho la Michezo Tanzania alisema ana furaha kubwa kwa ushirikiano baina ya pande hizo mbili.

“Ni furaha kubwa kushiriki katika uzinduzi wa ushirikiano wa pande hizi mbili, Zantel na United Against Malaria, na kwa hakika utasaidia katika kuendeleza juhudi za kupambana na Malaria hatimaye kufikia lengo la Tanzania Bila Malaria’’ alisema Tenga.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: