Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi

Wilaya ya Handeni mkoani Tanga, inakabiliwa na upungufu mkubwa wa Walimu wa Masomo ya Sayansi katika shule zake za sekondari wilayani humo.

Akizungumza kwa njia ya simu, Afisa Elimu ya Sekonda wilayani Handeni Mwl. Simon Mdaki, wakati wa mahojiano maalumu na Mwandishi wa habari hizi ofisini kwake.
Mwl. Mdaki alisema kuwa wilaya ya Handeni yenye jumla ya shule 31 za Sekondari zikiwemo 29 za Serikali na mbili za binafsi, ina Walimu 58 tu wa masomo ya sayansi wakati ambapo mahitaji ni walimu 158 na hivyo kuwa na upungufu wa walimu 100.

Amesema kati ya walimu 125 wa Sekondari waliopelekwa Handeni mwaka huu kufundisha katika shule mbalimbali wilayani humo, ni walimu saba tu wenye fani ya masomo ya Sayansi jambo ambalo amesema bado ni kikwazo kwa somo hilo kupatiwa ufumbuzi wa kudumu.

Mwl. Mdaki alisema kuwa uhaba wa walimi wa masomo ya Sayansi wilayani Handeni, umechangia kwa kiasi kikubwa kupunguza ufaulu wa wanafunzo kwa somo hilo katika mitihani yao ya taifa mwaka jana.

Alisema ni asilimia 30 tu ya wanafunzi wa kidato cha nne waliofanya vizuri katika somo hilo mwaka jana ambapo asilimia 70 kati yao walifeli jambo ambalo limeleta changamoto kubwa na kuifanya wilaya hiyo kujipanga upya kubabiliana na hali hiyo ili kuongeza kiwango cha ufauli baadaye mwaka huu.

Mwl. Mdaki amelitaja tatizo lingine linalozikabiri shule nyingi za Sekondari wilayani humo kuwa ni ukosefu wa vyumba na vifaa vya maabara kwa ajili ya wanafunzi kujifunzia mambo kwa vitendo badala ya nadharia pekee.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Handeni Bw. Muhingo Rweyemam akizungumzia tatizo hilo, amesema kuwa Serikali imepeleka maabara ya sayansi inayojongea (Mobile Laboratory) katika shule nne za sekondari zenye walimu wa Sayansi.

Bw. Rweyemamu amezitaja shule hizo zenye maabara inayojongea kuwa ni Kwamsisi, Kang’anta, Kwankonje na Ndolwa, maabara ambazo zitawawezesha pia wanafunzi wa shule jirani kusoma kwa vitendo masomo ya sayansi wakati serikali zikiendelea na hatua zingine za kumaliza tatizo hilo.

Amesema kwa kutumia mapato ya ndani ya Halmashauri, Wilaya ya Handeni imeanzisha utaratibu wa kujenga maabara ya sayansi katika shule za Sekondari Chogo iliyopo tarafa ya Mkumburu na katika sekondari ya Mazingara iliyopo tarafani humo.

Lakini pia amesema kuwa kuna fedha za mpango wa maendeleo ya eluimu ya Sekondari MMES II ambazo sasa zinatumika kujenga maabara katika shule ya Sekondari Sindeni iliyopo katika tarafa ya Sindeni na Kisaza iliyopo katika Tarafa ya Mzundu wilani humo ujenzi amba unatarajiwa kukamilika baadaye mwaka huu.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: