Serikali nchini Kenya imetangaza kufungwa kwa shule zote za msingi za umma huku walimu wa shule za umma za msingi na sekondari wakisitisha mgomo wao.

Waziri wa elimu profesa Profesa Jacob Kaimenyi alisema kuwa shule hizo zitabakia kufungwa kwa muda usiojulikana. Ameshutumu walimu akisema kuwa mgomo wao ulikuwa kinyume cha sheria.

Zaidi ya walimu laki mbili na arobaini wamesusia kutoa mafunzo kwa wanafunzi wakidai nyongeza ya asili mia mia tano ya mishahara waliyoahidiwa na serikali mwaka wa 2007.

Pia wanataka kuongezewa marupurupu ya usafiri, ya nyumba na matibabu. Serikali ilisema kuwa wazazi wataarifiwa juu ya siku ya kufunguliwa tena shule.

Waziri huyo wa elimu alisema kuwa wizara yake itafanya mipango maalum kwa ajili ya wanafunzi wa darasa la nane wanaotarajiwa kufanya mtihani wao wa kitaifa chini ya miezi minne ijayo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: