Maandalizi ya Harusi Fashion Show 2013 yapamba moto, Maonesho hayo ya mavazi na wafanyabiashara wa bidhaa na huduma za harusi yanatarajiwa kufanyika tarehe 6 mwezi wa saba katika hoteli ya Hyatt Kilimanjaro, Dar es salaam. Muanzilishi na muandaaji wa Harusi Fashion Show Mustafa Hassanali amesema ikiwa ni mwaka wake wanne maonesho haya yamekuwa na kuongezeka ubora ukilinganisha na miaka iliyopita halikadhalika tunatarajia kuona mabadiliko kwenye tasnia ya Harusi na washikadau wake.

Mwaka huu Harusi Fashion Show tayari imeshawavuta washiriki wengi, wengi wao ni washiriki ambao wapo toka kuanzishwa kwa maonesho haya mwaka 2010 ambapo mwaka huu yanatarajiwa kufanyika kuanzia saa moja kamili joini na kuendelea.

“Harusi ni muunganiko wa familia na jamii na nikumbukumbu muhimu ya itakayodumu maisha yote, hivyo basi tumeamua kuwapa bibi na bwana harusi watarajiwa mahitaji yao yote ya siku hiyo muhimu kwenye hitoria ya maisha yao.” Amesema ndugu Esi Mgimba Afisa Habari na Mahusiano.

Harusi Fashion Show inawaleta pamoja wadau wa biashara za harusi ili waweze kukutana kufahamiana na kuangalia fursa za kibiashara baina yao ili waweze kuzitumia kuboresha biashara zao na uhusiano wa kibiashara ambao utachangia kukuwa kwa tasnia hii.

Miongoni mwa washiriki amabao watakuwepo mwaka huu ni pamoja na keki, maua na wapambaji, wapiga picha, wabunifu wa mavazi ya harusi na wengineo wengi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: