Kampuni ya Tigo Tanzania, kwa mara nyingine tena leo imehaidi kuunga mkono suala muhimu la maadhimisho ya siku ya uchangiaji damu kwenye siku ya dunia ya wachangiaji damu yatakayofanyika mkoani Mara tarehe 14 Juni, 2013. Zoezi hili lakuchangia damu yatafanyika katika mikoa yote hapa nchini yetu ambapouzinduzi wa mpango hu wa taifa hutafanyika mkoani mara kitaifa zitafanyika mkoani Mara nakuendelea katika mikoa mengine hapa nchini.
“Huduma ya kuchangia damu kwa mara nyingine imevutia kufanyiwa kazi na Tigo katika juhudi za kuinua uelewa wa jamii juu ya umuhimu wa kujitolea kuchangia damu katika kuhakikisha upatikanaji wa damu salama na ya kutosha.
Zoezi hili la uchangiaji wa damu litarajia kupunguza, kwa kiasi kikubwa, uhaba wa damu uliopo hivi sasa unaozikabili hospitali nyingi nchini, na kwa maana hiyo kuwezesha kuzuia vifo visivyo vya lazima, hususa, kwa wanawake na watoto ambao ndio wahitaji wakuu wa damu…. Ningependa kuchukua fursa hii kuishukuru kampuni ya Tigokwa msaada wake imara kwenye mpango huu unaolenga kuwapatia Watanzania maisha bora na yenye afya”. Alisema Dk. Efesper A. Nkya, program meneja wa mpango wa NBTS.
Afisa Mahusiano ya Jamii na Matukio wa Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo , Woinde Shisael alisema; “Kampuni ya Tigo inajisikia fahari kwa kuwemo kwake katika mpango huu wenye lengo la kuelimisha umma kuhusu umuhimu wa uchangiaji damu salama, huku tukiwashukuru wachangiaji damu waliopo na pia kutoa wito kwa wachangiaji wapya kujitokeza kuchangia damu. Afya ya jamii ni muhimu sana kwa kampuni ya Tigo na hivyo kuifanya Tigokujihususha kikamilifu katika mpango huu. Hili ni jambo linalohitaji msaada wa kila mmoja wetu”.
Shisael aliongeza kusema kwamba; “ Napenda kuchukua fursa hii kuwaomba Watanzania wote kuipa muhimu unaostahili suala hili na kujitokeza kuchangia damu na hivyo kuokoa maisha ya wahitaji kama kaulimbiu ya mwaka 2013 inavyosema “Kila mchango wa Damu ni zawadi kwa maisha”. Tigo itaendelea kushirikiana na kuwekeza katika sekta ya afya nchini kwajili yakuhakikisha kwamba Watanzania wote wanaendelea kua na afya nzuri.
Siku ya uchangiaji damu duniani ni mpango uliobuniwa ili kuelimisha kuhusu umuhimu wa damu salama, kuhamasisha uchangiaji damu wa hiyari na pia kuwashukuru wachangiaji damu bila malipo kwa mchango wao mkubwa katika kuokoa maisha. Kaulimbiu ya kampeni ya dunia ya uchangiaji damu 2013 inasema “Kila mchango wa Damu nikama zawadi wa maisha kwa binadam”.
Toa Maoni Yako:
0 comments: