20130616-154106.jpg

Ndugu wanajumuiya, Kamati ya msiba Inapenda kuwashukuru Wanajumuiya wa Houston, watanzania waishio nje ya Houston na watu wa mataifa mengine kwa kufanikisha shughuli ya harambee ya kukusanya pesa za kusafirisha mwili wa marehemu Jerome kuelekea nyumbani Tanzania.

Mmeonyesha moyo mkubwa wa upendo na ushirikiano na tunawaomba muendelee na moyo huo.

Tunatarajia kusafirisha mwili wa marehemu kwenda nyumbani Tanzania Alhamisi (06/20/2013) au Ijumaa (06/21/2013).

Kutakuwa na misa ya kumuombea marehemu pamoja na kutoa heshima za mwisho siku ya Jumanne Tarehe 18 mwezi wa sita (06/18/2013)

Mahali na muda ni kama ifuatavyo hapo chini:
Address:
St. Cyril of Alexandria Catholic Church
10503 Westheimer Rd.
Houston TX 77042
Phone: 713-789-1250
Muda:
3:00 PM – 4:00 PM Viewing
4:00 PM – 5:30 PM Misa
5:30 PM – 6:00PM Viewing

Note:
Shughuli itaisha 6:00PM (kanisa linafungwa muda huo).
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: