Mkuu wa mkoa Rukwa Eng. Stalla Manyanya kushoto akimfariji msanii na taarab na malkia wa mipasho Tanzania Khadija omar Kopa alipokua kwenye chumba maalum cha kupumzikia wageni kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda baada ya kupewa taarifa ya kufiwa na mumewe Jafari Ali Yussuf aliyefariki Dunia leoa alfajiri kutokana na ugonjwa, Bi Khadija Kopa alikua akitokea kwenye maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani kitaifa yaliyoaadhimishwa Namanyere Mkoani Rukwa jana.

Baadhi ya viongozi na wananchi wa mkoa wa Rukwa na Mpanda wakimsindikiza kuapanda ndege msanii wa taarab na malkia wa mipasho Tanzania Khadija Omar kopa kwenye uwanja wa ndege wa mpanda baada ya kupewa taarifa ya kufiwa na mumewe Jafari Ali Yussuf aliyefariki Dunia leo alfajiri kutokana na ugonjwa, Bi Khadija Kopa alikua akitokea kwenye Maadhimnisho ya siku ya Mazingira Duniani kitaifa yaliyoadhimishwa Namanyere Mkoani Rukwa jana. (Picha na ofisi ya Makamu wa Rais).

Taarifa zinaeleza kuwa Mume wa Mwanamuziki Mkongwe wa Miondoko ya Taarab, Malkia wa Mipasho, Bi. Khadija Kopa, aitwaye Jaffari Ally amefariki dunia usiku wa kuamkia jana majira ya saa 9 usiku.

Akidhibitisha juu ya msiba huo, zimetolewa na Katibu wa Bendi ya TOT, Gasper Tumaini.

Chanzo cha kifo chake ni ugonjwa wa Malaria, ambapo siku ya Jumatatu marehemu Ally alipelekwa Hospitali ya Lugalo kwa ajili ya kupata matibabu.

Marehemu alipata nafuu na kurudi nyumbani kwao Bagamoyo, hali ambayo ilimpelekea Khadija Kopa kusafiri kikazi, na inasemekana mpaka umauti unamkuta Jaffari, Mkewe Khadija Kopa alikuwa yupo kikazi mikoani kwa ajili ya shughuli zake za kimuziki.

Marehemu Jafary Ally anazikwa leo saa tisa mjini huko mjini Bagamoyo.

Kwa sasa msiba upo kwa wazazi wake Tandale, lakini muda mchache ujao watu wataanza kuelekea Bagamoyo kwa ajili ya mazishi. Jana kulikuwa na mvutano, baada ya baadhi ya watu, wakiwamo viongozi wa CCM kutaka Ally akazikwe Bagamoyo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: