Na Mwandishi Wetu

MKALI wa muziki wa kizazi kipya nchini, Naseeb Abdul ‘Diamond Platinum’ ameisambaza video ya ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Ukimwona’ ambayo inafanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Diamond alisema kazi hiyo ameisambaza juzi katika vituo mbalimbali vya televisheni na kwamba anaamini itafanya vizuri kutokana na ubora wa mazingira aliyotumia kushuti video hiyo.

“Najua mashabiki wangu wananijua vizuri sijaja kuuza sura mjini, naomba mashabiki wangu wakae mkao wa kula kwajili ya kuzipokea kazi zangu zingine zinazofuata kwani nina mashairi mengi yanasubiri muda tu wa kuingia mtaani,” alisema.

Diamond ni kati ya wasanii ambao wanafanya vizuri katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya huku akitamba na baadhi ya ngoma zake kama Kesho, Mapenzi basi, Ritha na nyinginezo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: