Diamond akilonga na Sauda kuhusu shoo kali atakayotoa Usiku wa Matumaini
Sauda na Diamond wakiwa mbele ya kamera.
Platnumz akijiaandaa kabla ya mahojiano.
...Akibadilishana mawazo na Sauda kabla ya kuanza mahojiano.
Mtu wa kamera akiwa mzigoni.
Na Wilbert Molandi

MKALI wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond’ ametamba kufanya shoo kali ikiwemo kumfunika msanii wa Uganda, Prezzo katika Tamasha la Matumaini 2013 litakalofanyika Sikukuu ya Sabasaba kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.

Diamond ametoa majigambo hayo wakati wa mahojiano na Mtangazaji wa kituo cha Star TV, Sauda Mwilima.

“Nimeahidi kufanya bonge la shoo kwenye Tamasha la Matumaini siku hiyo, mashabiki wangu na wapenzi wa muziki wajitokeze kwa wingi.

“Ninataka kudhihirisha ubora wangu siku hiyo kwa kumfunika vibaya Prezzo,” alisema Diamond.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: