Msafara wa Kamishina Jenerali wa Magereza CGP John C. Minja ukiwasili katika viwanja vya Chuo cha ufundi Ruanda Jijini Mbeya kwa ajili ya kuwatunuku nishani Maaskari wa Jeshi la Magereza
Kamishina Jenerali wa Magereza CGP John C. Minja Akikagua Gwaride maalum lililoandaliwa na maaskari wa Jeshi la Magereza kwa ajili yake mara baada ya kuwasili katika viwanja hivyo kwa ajili ya kuwatunuku nishani Maaskari.
Kamishina Jenerali wa Magereza CGP John C. Minja akipokea Salam za heshima kutoka kwa Askari wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Mbeya.
Baadhi ya Maaskari wa Jeshi la Magereza wakitoa heshima kwa Kamishina Jenerali wa Magereza CGP John C. Minja (ambaye haonekani pichani) wakati wa hafla ya kuwatunuku nishani.
Brass band ya Jeshi la Magereza kutoka Kiwira Rungwe wakitumbuiza katika Sherehe hizo.
Baadhi ya Maaskari wastaafu wa Jeshi la Magereza pamoja na maofisa wakifuatilia kwa umakini Sherehe za kutunuku nishani
Baadhi ya Maaskari wakisubiri kutunukiwa nishani kutoka kwa Kamishina Jenerali wa Magereza CGP John C. Minja
SACP C. A Keenja akitaja majina 29 ya Maaskari wanaotakiwa kutunukiwa Nishani ya Utumishi uliotukukuka Tanzania, Utumishi Muda Mrefu Tanzania, Utumishi mrefu na tabia njema na Mwenge wa Uhuru daraja la nne.
Askari Mwanamke akitembea kwa ukakamavu kuelekea eneo linalotumika kutunukia Nishani kwa Maaskari wa Jeshi la Magereza.
Kamishina Jenerali wa Magereza CGP John C. Minja (kulia) akimvisha nishani ya utumishi ulio Tukuka Tanzania ACP Hawa M. Simon ambaye pia ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Rukwa.
Kamishina Jenerali wa Magereza CGP John C. Minja akimvisha Nishani ya utumishi mrefu na tabia njema SGT Yusufu F. Nzunda kutoka chuo cha Magereza Kiwira
Kamishina Jenerali wa Magereza CGP John C. Minja Akimpongeza Askari mara baada ya kutunukiwa nishani ya utumishi mrefu na Tabia njema.
Kamishina Jenerali wa Magereza CGP John C. Minja Akiwa katika picha ya pamoja na Maaskari 29 waliotunukiwa Nishani mbalimbali
Kamishina Jenerali wa Magereza CGP John C. Minja akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Maofisa wa Jeshi la Magereza wastaafu.
Kamishina Jenerali wa Magereza CGP John C. Minja akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanawake waliotunukiwa Nishani
Kamishina Jenerali wa Magereza CGP John C. Minja akibadilishana jambo na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Barakael Masaki
Kamishina Jenerali wa Magereza CGP John C. Minja akiwa katika picha ya Pamoja na Afisa Habari wa Jeshi la Magereza Makao Makuu Insp. Lucas Mbonje wakizungumza na waandishi wa Habari mbalimbali wa Mkoa wa Mbeya.
---
RAISI wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewatunuku Nishani mbali mbali Askari 29 kwa Askari wa Jeshi la Magereza kutoka Nyanda za juu kusini.
Mbali na Nishani hizo pia Jeshi hilo limesema limejipanga kuhakikisha linaanza kujitegemea na kuepukana na Bajeti za Serikali katika kujiendesha kutokana na uwepo wa Rasilimali nyingi zinazoweza kuzisaidia hususani Wafungwa na Ardhi kwa ajili ya kuzalisha Chakula.
Toa Maoni Yako:
0 comments: