Mkurugenzi wa Mipango wa British Council Tanzania, Andrew Piner (Kushoto) akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juu ya uzinduzi wa mashindano ya watoto wa Mazingira magumu yanayotarajiwa kufanyika jijini Brazil mwakani. Pembeni yake ni Mwakilishi wa Rotary Club ya Bahari Beach, Mkurugenzi wa Kituo cha Tanzania Street Children Sports Academy pamoja na Erica Campayne kutoka shirika la LIFT nchini Marekani ambao wanasimamia upande wa kuwafundisha walimu na wakuu wa vituo vya watoto wenye mazingira magumu jinsi ya kutambua uwezo wa watoto ili waweze kujieleza, kutumia vipaji vyao
tofauti na mpira.
Mkurugenzi wa Kituo cha Tanzania Street Children Sports Academy ambao ni waandaaji wa mashindano hayo ya watoto wa wanaoishi katika mazingira magumu akielezea juu ya mchakato wa kutafuta watoto watakaoshiriki kuunda timu ya Taifa itakayoshiriki katika mashindano yatakayofanyika nchini Brazil. Kwa mara ya kwanza tumepanua wingo wa kuja jijini Dar es Salaam ili kuunganisha na jiji la Mwanza. (Pembeni yake ni Mwakilishi wa Rotary Club ya Bahari Beach, na Erica
Campayne kutoka shirika la LIFT nchini Marekani).
Aliongeza kuwa katika mashindano yaliyofanyika nchini Afrika Kusini mwaka jana Timu ya Tanzania iliweza kuchukua nafasi ya tano baada ya kuzichakaza timu za Brazil, Ufilipino, Karagwa na Uingereza ambayo tulitoka sare.
Mwaka huu timu zinazoshiriki mashindano hayo zipo 16 na kwa Bara la Afrika zipo timu 7 ambazo ni Kenya, Burundi, Libya, Sea-lion, Egypt, Afrika Kusini na Tanzania pia alisema kuwa jumla ya Mabara manne yanatarajia kushiriki.
British Council Tanzania pamoja na Rotary Club ya Bahari Beach ndiyo wadhamini wa michakato yote ya kusimamia Semina, pamoja kuiwezesha timu kuundwa.
Waandishi wa Habari wakifuatilia.
Mkurugenzi wa Kituo cha Tanzania Street Children Sports Academy akijibu maswali ya waandishi wa habari.
Walimu na wakuu wa vituo vya watoto wanaoishi katika mazingira magumu vya jijini Dar wakiwa katika semina kuwafundisha jinsi ya kutambua uwezo wa watoto ili waweze kujieleza, kutumia vipaji vyao
tofauti na mpira.
Wakimsikiliza mkufunzi.
Wakiwa makini kufuatilia mafunzo wanayoyapata.
Mkufunzi akitoa maelekezo jinsi ya kufanya.
Mkufunzi akitoa mafunzo kwa vitendo juu kuwajengea uwezo watoto wao na kutambua vipaji walivyonavyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments: