Imeandikwa na Haika Lawere
Huwa katika maisha ya kila siku kuna watu ambao ni kama wanakimbilia katika maisha, yaani ni kama watu wamekaa foleni benki halafu wewe unakuja, unawapita unaenda moja kwa moja kwa cashier unataka akuhudumie eti una haraka, na matokeo yake unarudishwa nyuma usubiri zamu yako.
Sasa basi nimekuwa nikiona watu wakijaribu kila mbinu duniani, iwe kuonea wengine, kuwabania wengine, kuchonganisha, Fitina, kutoa miili yao, uchawi, kuiba, forgery, fraud, kutapeli, kuuwa na kufanya kila shortcut ili wafike faster kule waendako, na wakati mwingine huwa wanafika LAKINI ni kama creator (Mungu) anasema NO!NO!NO! haukuwa muda wako kuwa namba 1, 2, 3 rudi nyuma ukaanze tena foleni ikifika zamu yako nitakupa tena na ziada kama ukitaka!!
Nimeliona kwa watu wengi sana, wana nyanyuka ghafla from nowhere!!! and then from nowhere wana-fall ghafla like, hell! ghosh! Jamani life ni Process/Maendeleo ni process/kusoma ni process it takes time kufikia achievements halali zote hapa duniani, ila ukivumilia, success yako inakuwa ni ya Halisi na ya kudumu na hutoangushwa kirahisi! God bless u all dear friends!!
Toa Maoni Yako:
0 comments: