Mtaalam wa sheria za kimataifa na Haki za Binadamu kutoka mtandao wa kimataifa wa wabunge wanaotetea Haki za Binadamu, Amani na Utawala wa Sheria duniani Bw. Peter Barcroft (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu mkutano wa wabunge walio kwenye mtandao huo jijini Dar es salaam kujadili namna watakavyounganisha nguvu zao katika kuzihamasisha na kuzishawishi nchi mbalimbali duniani kupinga na kuzuia silaha kuangukia mikononi mwa makundi ya wahalifu kwa kusaini mikataba inayozuia hali hiyo.
Mbunge kutoka Ghana Bw. Alban Bagbin akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa mkutano wa wabunge walio katika mtandao wa Kimataifa wa kutetea amani, maendeleo, utawala wa sheria na Haki za Binadamu duniani watakavyopanga mikakati mbalimbali ya kuzishawishi nchi wanazotoka kusaini mikataba inayozuia uagizaji , uingizaji na usambazaji wa silaha katika nchi zao kuyafikia makundi yasiyohusika ambayo yamekuwa chanzo cha uvunjifu wa amani duniani. Takribani wabunge 22 kutoka nchi za Afrika wanashiriki mkutano huo.
Mbunge kutoka Sierra Leone Bernadette LAHAI akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani) athari zinazosababishwa na silaha kuangukia katika mikono ya wahalifu hasa katika bara la Afrika na kuwa chanzo cha machafuko na kukwamisha maendeleo ya wananchi.

Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: