Kifo cha msanii Albert Mangwea kimesababishwa na utumiaji wa madawa ya kulevywa uliokithiri.

Kwa mujibu wa ripoti kutoka katika hospitali ya St. Hellen, Johannesburg Afrika Kusini na washikaji zake wa karibu zinasema marehemu alitumia madawa ya kulevywa kupita kipimo (overdose) na kupelekea kifo chake.

Rafiki zake hao ambao hawakupenda kutaja majina yao walisema kuwa kiukweli Msanii huyo alikuwa akitumia madawa ya kulevywa kwa muda mrefu na wakati mwingine amekuwa akitumia madawa hayo bila kula hiyo kumfanya mwili wake kudhoofika jambo ambalo lilikuwa likiatarisha afya yake.

"Msanii huyu na mwenzake M to The P walikuwa na mualiko wa kufanya show huku Afrika Kusini na walitakiwa kuondoka leo (jana) kurudi Dar saa tatu asubuhi, lakini baada ya kuona hawatokei ndio tukaamua kwenda walipokuwa wamefikia na kuwakuta wote wawili wakiwa hawajielewi baada ya kujidunga madawa ya kulevya mengi (overdose), ndipo tulipochukua jukumu la kuwakimbiza hospitali, habari ndio ikawa Ngwea amefariki na M to the P yuko hoi bado hajitambui hospitali, japo kiukweli hata tunampeleka hospitalia alikuwa tayari amefariki japo dokta ndiyo alitakuwa kuthibitisha hilo.

Hata hivyo mama yake Ngwea ambaye yupo nyumbani kwao Morogoro amethibitisha kupokea taarifa ya kifo cha mwanae na kusema kuwa taarifa za kuwa za kuwa alikuwa Afika Kusini alikuwa hana kwani mara ya mwisho kuongea naye zimepita wiki mbili sasa.

Pia amesema taratibu za maandalizi ya mazishi yatakavyokuwa yataanza baada ya kufika baba yake mdogo Ngwea ambaye yupo mkoani Ruvuma kwani anatarajiwa kuwasili leo Morogoro.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: