
Meneja
Uhusiano wa MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi akiwakaribisha
wageni wanahabari katika hafla mchapalo ya kusheherekea Africa Day na
Dstv ambapo alisema DStv inatoa nafasi kwa wateja wake kuwa na fursa ya
kuchagua vifurushi mbalimbali kulingana na uwezo wa mteja ambacho cha
uwezo wa chini kabisa ni Access chenye zaidi ya channeli 40 gharama yake
ni nafuu sana ambapo mteja atalipia shilingi 16,500 kwa mwezi.

Meneja wa Fedha wa kampuni ya Multichoice Tanzania, Bw. Francis Senguji
akizungumzia malengo ya DStv Tanzania ambapo amesema wao kama
waendeshaji wa biashara nyingine barani Afrika wanaojali na kuthamini
maendeleo ya jamii wameona ni wajibu kusaidia jamii ili kuweza
kuendeleza maendeleo ya kijamii nchini Tanzania.
Kwa
kuendeleza hilo Multichoice ina mfumo wa kutoa elimu mashuleni (Multichoice Resource Centre) hivyo watamumia jukwaa la Teknolojia kama
darasa kwa njia mbalimbali kuwapa jamii nafasi ya kuendeleza vipaji na
ujuzi.
Mfumo
huo kutoa rasilimali kwenye shule kama vile ving'amuzi vya Satellite,
VCRs/DVD na kifurushi cha elimu cha Dstv. Mpaka sasa Multichoice
imeanzisha vituo vya rasilimali jamii katika shule 82 nchi nzima kwenye
mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Iringa, Kagera, Mbeya, Pwani na
Tanga.

Meneja
Uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo (katikati)
akifafanua jambo wakati wa hafla mchapalo katika kusheherekea usiku wa
Africa Day na DStv. Kulia ni Meneja Masoko wa Kampuni hiyo Furaha Samalu
na kushoto ni Meneja Uhusiano wa Kampuni hiyo Barbara Kambogi.
Viongozi wa DSTV wakibadilishana mawazo na wadau.

Barbara Kambogi akiteta jambo na Angela Msangi wa TBC.

Kutoka
kushoto ni Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania Furaha Samalu, Blogger
John Bukuku wa Fullshangwe Blog, Meneja Uendeshaji wa kampuni hiyo
Ronald Shelukindo, Mdau wa DStv na Meneja wa Fedha katika kampuni hiyo
Bw. Francis Senguji wakipozi kwa picha.

Meneja
Uhusiano wa MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi (kulia) akifurahi
jambo Wanahabari Sidi Mgumia (katikati) na Mama Mhina.
Ronald Shelukindo na Mdau LEMUTUZ wa Blog ya jamii.

Kutoka
kushoto ni Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania Furaha Samalu, Meneja
Uendeshaji wa kampuni hiyo Ronald Shelukindo, Meneja wa Fedha katika
kampuni hiyo Bw. Francis Senguji na mdau wa DStv wakipozi mbele ya
camera yetu wakati wa hafla ya kusheherekea African Day na DStv
iliyowakutanisha waandishi wahabari kutoka vyombo mbalimbali nchini.

Wanahabari
wakiwa bize kujaza Quiz iliyotolewa na kampuni ya Multichoice Tanzania
ambapo mshindi kwanza amezawadiwa Full Set ya King'amuzi cha Dstv na
'Subscription' ya mwezi mmoja na washindi kumi wamezawadiwa kofia na
T-shirts za Supersport moja ya chaneli zinazopatikana katika king'amuzi
cha Dstv.
Waandishi wa habari kutoka katika magazeti tando, John Bukuku (mwenye tshrt ya mistari) akiwaonyesha kitu wenzake.
Gumzo la hapa na pale likiendelea.
Mhasibu Mkuu wa Kampuni ya Multichoice Tanzania, Francis Senguji akizungumza katika hafla hiyo.

Wanahabari wakiendelea kuumiza kichwa huku wengine waki-google majibu ya Quiz hiyo kupitia simu zao za kiganjani.

Mtangazaji
wa Radio Dennis Buslwa a.k.a Ssebo (kulia) akiwa busy kutafuta majibu
ambapo tunahisi alikwa anawasiliana na watu wa Mo Blog wampe majibu
kamili. Wengine ni Kamera Man wa Channel Ten na Mtangazaji wa Radio
Salma Msangi pamoja na mdau wa Star Tv.

Dada Revina Bandihai wa kampuni ya Multichoice Tanzania na HR Manager wa kampuni hiyo.

Ronald Shelukindo na Dada Furaha Samalu wakifungua mziki wa Kiafrika huku Bw. Francis Senguji akiserebuka na mdau.

Mkurugenzi
wa Fullshangwe Blog John Bukuku akiserebuka na Meneja Uhusiano wa
Multichoice Tanzania Barbara Kambogi wakati wa hafla hiyo.

Salma Msangi akionekana Kiafrika zaidi akiyarudi na Khadija Kalili wa Tanzania Daima.


Kutoka
kushoto ni Blogger Cathbert Angelo wa kajunason Blog, Mpiganaji Fadhili
Akida na Blogger Othman Michuzi wa Mtaa kwa Mtaa.

Bloggers katika picha ya pamoja.
Dada Revina Bandihai wa Multichoice Tanzania na Bw. Francis Senguji wakisataka Rhumba wakati wa hafla hiyo.
Meneja wa Fedha wa Multichoice Tanzanua Bw. Francis Senguji akimpongeza
Ssebo baada ya kuibuka mshindi katika Quiz iliyoendesha na Kampuni hiyo
ambapo alinyakua Full Set ya King'amuzi cha Dstv na 'Subscription' ya
mwezi mmoja.

Pichani
juu na chini Meneja Uhusiano wa Multichoice Tanzania Barbara Kambogi
akigawa Kofia na T-shirts kwa washindi wa Quiz ilyoendeshwa na kampuni
hiyo wakati wa kusheherekea Africa Day na Dstv.


Dada Revina Bandihai (kushoto) wa Multichoice Tanzania akishow love na washindi wa Quiz iliyoendeshwa na kampuni hiyo.




Toa Maoni Yako:
0 comments: