Diwani wa kata ya Tunduma Bw. Frank Mwaijoka (Chadema) pamoja na mchungaji wa kanisa la Kanisa la Kiinjili la Kirutheri Tanzania katika eneo la Tunduma wilayani Momba Mkoani mbeya wametakiwa kujisalimisha kituo cha Polisi Tunduma mara baada ya kuhusika na uchochezi wa kidini hali ambayo imepelekea kutokea kwa vurugu.

Vurugu hizo ambazo zilianza majira ya saa 3:00 asubuhi katika eneo hilo mara baada ya kundi la watu wanaodai kuwa wao ni wafuasi wa dini ya kikristo wakidai waruhusiwe kuchinja mifugo na kuuza katika mabucha yao hali iliyo pelekea kuibuka kwa vurugu hizo.
Matairi yanachomwa katikati ya barabara.
Wananchi wakiwa na jazba.
Mambo hayo ya mabuta ya nyama.

Askari wakiwatuliza wananchi.
Mwandishi wa Mbeya yetu pamoja na waandishi wenzake walipata shida sana kufika mji wa Tunduma walikutana na vikwazo vingi sana lakini wananchi walikuwa waelewa waliwasaidia kutoa magogo na matairi ili wapite wakapate habari.
Askari wakitoa magogo barabarani ili waweze kupita.
Mitaa ikiwa haina watu wamekimbia biashara zao.

Wananchi wakikimbia wasijue pa kwenda baada ya hali ya hewa kuchafuka kutokana na vurugu.
Ulinzi ukiimalishwa.


Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya, Diwani akiongea na waandishi wa habari.
Polisi wakiendelea kazi yao katika mitaa ya Tunduma
Hali ya usalama ikisimamiwa ipasavyo na vijana wa kazi.
---
Akizungumza kuhusiana na tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoani humo, Diwani Athumani alisema kuwa kufuatia kuwepo kwa tukio hilo jumla ya watu zaidi ya 40 tayari wamekwisha kamatwa.

Alisema mpaka sasa taarifa walizo zipata kufuatia vurugu hizo zinaeleza kuwa miongoni mwa watu walichochea vurugu hizo ni diwani wa kata hiyo ya Tunduma, John Mwaijoka pamoja na Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kirutheri Tanzania, Neema Mwaipusa ambao kwa pamoja wametakiwa kujisalimisha kituo cha polisi kwa mahojiano zaidi.

Alisema suala hilo limegubikwa na siasa kwani tayari viongozi wa serikali akiwemo Mkuu wa mkoa huo, Bw. Abbas Kandoro amekwisha litolea ufafanuzi Aprili 02 mwaka huu wakiwepo pia viongozi wa dini.

Aliongeza kuwa asilimia kubwa mgogoro huo juu ya nani achinje umeingiliwa na mambo ya kisiasa kwani hata baadhi ya wananchi wa maeneo hayo wamekuwa wakilalamika juu ya kutokea kwa vurugu hizo.

Shughuli za kibiashara katika eneo hilo zimeshindwa kufanyika katika hivyo kufanya wananchi kupata adha hasa kwa nchi jirani ya Zambia ambao kwa asilimia kubwa wanategema kupata mahitaji kutoka mpakani mwa Tanzania.

Hata hivyo Diwani alisema kuwa katika vurugu hizo askari mmoja pamoja na mwananchi wamejeruhiwa kwa kupigwa mawe ambapo tayari wamekwisha fikishwa kituo cha polisi.

Kufuati hali hiyo Kamanda wa Polisi, alisema kwa sasa hali imelejea katika hali yake ya kawaida hivyo amewataka wananchi wa maeneo hayo kuwa watulivu wakati jeshi hiulo la Polisi likiendela na msako wa kuwatafuta wahalifu wengine.

Picha/Habari na Mbeya Yetu
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: