Wasanii wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kufanya usafi katika makaburi  ya wahanga wa MV. Bukoba.
Msanii wa Kizazi kipya, H.Baba akiwajibika.
Kazi ya kufanya usafi ikiwendelea.
Na Albert G. Sengo, Mwanza

Wasanii wa muziki wa kizazi kipya (Bongo Fleva) Kala Jeremiah, H. Baba, Kitale na mwanadada Dyna leo wameshiriki zoezi la kusafisha mazingira ya makaburi ya watu waliofariki dunia kwenye ajali ya kuzama kwa meli ya Mv. Bukoba, makaburi yaliyoko Igoma nje kidogo ya jiji la Mwanza.

Zoezi hilo limekuja mara baada ya mmoja kati ya wasanii hao (H. Baba) kupita katika eneo hilo na kujionea hali mbaya ya mazingira ndipo alipochukuwa jukumu la kuwasilisha taarifa hiyo kwa wasanii wenzake ambapo uungwaji mkono ulikuwa wa asilimia mia moja.

Mapema leo shughuli za usafi zilianza kushika kasi, zoezi ambalo liliwachukuwa takribani masaa manne kumalizika likuwa gumu kutokana na magugu na nyasi nyingi kumea kwenye eneo hilo la makaburi kiasi cha kuwasababisha wasanii hao kuongeza zana zaidi za usafi ili kuweza kufikia lengo lao.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: