Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe (Mwenye suti nyeusi),
akiteta jambo na Makamu Mwenyekiti wa Wakala wa Forodha na Uondoshaji
Shehena Tanzania(TAFFA) Bw. Edward Urio (kulia kwa Dkt Mwakyembe), leo
wakati wa mkutano wake na Wananchama wa wakala hiyo.
Wananchama wa Wakala wa Forodha na Uondoshaji Shehena Tanzania (TAFFA),
wakimsikiliza Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe (hayupo
pichani), Wakati alipokuwatana nao leo mchana katika ukumbi wa
Karimjeee. Waziri wa Uchukuzi amewaagiza wananchama hao kuhakikisha
wanawaondoa mawakala ambao wanawaharibia sifa yao.
Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe akisalimiana na Uongozi wa
wakala wa forodha na uondoshaji shehena Tanzania(TAFFA), mara baada ya
kuwasili katika ukumbi wa Karimjee kusikiliza kero walizonazo leo
mchana.
Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe akisisitiza jambo kwa wanachama wa wakala wa forodha na uondoshaji shehena Tanzania(TAFFA) leo Mchana wakati alipokutana nao katika ukumbi wa Karimjee.
Picha na Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini - UCHUKUZI


Toa Maoni Yako:
0 comments: