Naitwa Mwanaisha Nyange a.k.a Dayna (pichani) ni mwanamuziki wa muziki wa bongofleva ni mwanamke wa Kitanzania.  Napenda kuungana na wanawake wengine duniani kote katika kuhadhimisha siku ya wanawake duniani.

Nawashauri wanawake wenzangu juu ya kujituma kufanya kazi ili kujipatia maendeleo bila kutegemea wanaume. Naamini wenyewe tunaweza tena bila hata ya kuwezeshwa. 

Kupitia siku hii muhimu kwetu naiomba serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhakikisha inapambana vilivyo juu ya unyanyasaji wa kijinsia tunaoupata wanawake hasa ubakaji, ukeketaji na mauaji yanayoendelea dhidi yetu, tunaiomba serikali ihakikishe kwamba wahusika wa matukio kama hayo wanachukuliwa hatua za haraka ili kukomesha maovu hayo. 

Pia ni jukumu la kila mwanamke na niwajibu wetu kina mama pia na jamii kwa jumla kupambana na majanga haya. Tushikamane kujitetea. Tupendandane tushikamane, WANAWAKE TUNAWEZA.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: