Meneja wa kampuni ya Tigo, Bw. William Mpinga (kati) akifafanua kuwa kwa "Mara nyingine tena Tigo inaendelea kuweka tabasamu katika nyuso za thamani za wateja wetu kwa kuwapa fursa ya kujifunza na kuonja tamaduni mpya. Tunayo furaha kwa mara ya pili kuwa na shindano letu la Promosheni yetu bomba ya ‘Ascend Y200’ na kutangaza washindi mbalimbali ambao wataondoka hivi karibuni Dar-es-salaam kwenda China.
Muwakilishi wa michezo ya Bahati Nasibu nchini, Bw. Bakari Maggid (kushoto) akifafanua jambo kwa Meneja Ubunifu wa Ofa za Kampuni ya Tigo, Bw. David Sekwao na Meneja wa Tigo, Bw. William Mpinga wakati wakichezesha bahati nasibu ya promosheni ya Ascend Y200 kwa njia ya simu iliyozinduliwa rasmi mnamo Oktoba 2012, ambapo inayomuwezesha mteja kununua samrtphone yenye kiwango na hadhi ya aina ya Ascend Y200 kwa punguzo la hali ya juu. Bahati nasibu hiyo ilifanyikia kwenye hotel ya Holiday Inn, jijini Dar es Salaam.
Droo ya kwanza ya Promosheni ya ‘Ascend Y200’ ilifanyika mnamo Disemba 19, mwaka 2012, ambapo washindi wawili wenye bahati safari ya kutembelea miji mbalimbali mashuhuri nchini China zilizogharamiwa na Tigo. Kutakuwa na droo nyingine tano ambapo jumla ya washindi wawili watachaguliwa katika kila droo, na kufanya idadi yao kuwa jumla ya washindi kumi.”
Aliongeza kuwa, zawadi hiyo ya safari ya China kwa washindi hao itajumuisha, Malazi, posho ya chakula kwa siku 3 katika hoteli ya  Dragon Hotel iliyopo katika jiji la Guangzhou China, kutembelea vivutio mbalimbali kwa nusu siku jijini Guangzhou, mapumziko ya siku nzima katika milima ya Lotus nchini humo, pesa za matumizi binafsi kiasi cha Dola 200 za Kimarekani kwa kila mshindi pamoja na gharama zote za usafiri wa ndege.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: