Umoja wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari nchini MOAT wameitaka Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kuwachukulia hatua watendaji wote wanaotumia madaraka yao kuwafanyia vitendo vya kinyama waandishi wa habari wanaoonekana kufichua ubadhirifu wanaoufanya.
Akizungumza wakati wa Mkutano wa Wadau wa Vyombo vya Habari waliokutana Jijini Dar es Salaam kuzungumzia hali ya kuzorota kwa mazingira ya usalama wa wanahabari, Mwenyekiti wa MOAT Dk. Reginald Mengi alisema baadhi ya watumishi hao wamekuwa wakitumika kuwatesa waandishi kwa ajili ya maslahi yao binafsi, kisiasa na kiuchumi.
Ili kukabiliana na changamoto hiyo, Dk. Reginald Mengi aliitaka Serikali kulichukulia tukio la kuvamiwa na kuteswa kwa Mhariri Mtendaji wa New Habari, Absalom Kibanda kama chachu ya kukomesha vitendo hivyo ili kuifanya tasnia hiyo kuwa huru na inayotenda haki kwa jamii.
Baadhi ya wadau ambao wameshiriki mkutano huo wametumia fursa hiyo kutoa matamko yao mbalimbali ikiwemo Serikali kuunda tume huru ya wapelelezi kuchunguza kwa undani tukio la kutekwa na kuteswa kwa Kibanda ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri nchini TEF.
Toa Maoni Yako:
0 comments: