Kumekuwa na baadhi ya kero ambazo sijui kama zinanikera mimi peke yangu ama ni wadau wengi pia zinawakera, na moja ya mambo ambayo ni kero kwangu katika mji wangu wauitao manispaa ni MFUMO MBOVU wa ukusanyaji kodi za Halmashauri hasa za USAFI na PARKING  katika mji wa Bukoba.

Tokea kuletwa kwa Mkuu wa mkoa mpya Kanali Mstaafu Fabian Massawe (pichani), kumekuwa nahali ya dhati ya kuonekana kupatikana kwa mabadiliko katika Manispaa ya Bukoba hali ambayo nimekuwa nikiipenda japo naona kama imechelewa ila kwa wakati mwingine naamini kuwa imekuja katika muda muafaka kwani hata ujio wa taasisi za Elimu ya juu ndipo zaanza na nategemea kwa miaka kadhaa basi itakuwa na mafanikio na mabadiliko ya kweli kuonekana katika mkoa wenye sifa nyingi nje ila usio na yale wengi wanadhania kuwa nayo kwa sababu tu ya hali watu wa mkoa huu huonyesha wakiwa nje ya kwao.

Mh. Massawe tangu akiwa mkuu wa wilaya ya Karagwe amekua na  utaratibu maalum wa usafi katika wilaya hiyo katika siku ya Alhamis ambayo ilijulikana kama MASSAWE DAY ambayo hata alipopata ukuu wa mkoa amejitahidi kuisisitiza na kuifanya siku ya usafi hasa katika manispaa ya Bukoba.

Mh. Mkuu wa Mkoa. Ndg F. Massawe katika usafi

Tokea hapo, uongozi wa manispaa ukabuni mradi binafsi ambao kwa hakika ni kwa ajili ya kuwanufaisha wao wa kutoza pesa kwa ajili ya uegeshaji magari katika manispaa hali ambayo nadhani yanikera kuliko kitu chochote naweza sema.

 Kiutaratibu twajua kuwa kabla ya kuanzisha kitu ni vema kuandaa mazingira ili hata ukiiweka hicho kitu kiwe na manufaa kwako na kwa Umma, lakini wenzangu na mie hawa wamebuni kamradi binafsi haka na kutapakaza watu manispaa nzima wakitoza ushuru wa shilingi 500 kwa siku nzima bila hata kutoa elimu kwa "VIBARUA" hawa.
Parking za Manispaa zitozwazo kodi
Kwa kawaida tulitaraji kwanza kuona parking katika maeneo mbalimbali ndipo utoe elimu kwa Umma kuhusu pesa za parking na kuelimisha watoza ushuru wa Parking kujua ni baada ya muda gani wanastahili kumtoza mtu pesa. La kushangaza ni kwamba hakuna mahali popote katika manispaa ambapo pametengenezwa maalum kwa ajili ya parking ila Vibarua hawa wanatoza kodi na pangine hata kwenye maduka ambayo weenye majengo wanalipia kodi eneo lote.

Nikirudi kwenye suala la USAFI, huku nako naanza kuona dalili za kushindikana kwa jambo hili kwa kuwa watu hasa viongozi wa mitaa wamefanya hii programu kuwa kama njia ya kujipatia pesa za kiyabadili maisha yao. Nasema haya kwa sababu kuu moja nayo ni hii.

Katikasiku za hivi karibuni, Serikali ilianzisha mfumo mpya wa kuweza kujikusanyia mapato kwa kutumia vifaa maalumu ambavo wafanya biashara na Taasisi nyingi wanavitumia lakini kwa Halmashauri ya Manispaa hawana. Tozo la parking wapewa kijilisiti ambacho hata mimi naweza forge na kusema ni mtoza kodi na hivyo pesa nyingi kuishia kwa hawa watoza kodi,

ELCT Central office Parking

Tuachane na hilo, katika suala zima la usafi kuna adhabu zinatolewa kwa wanaokiuka utekerezaji wa agizo la Mkuu wa mkoa ambazo zinatofautiana kulingana na ukubwa wa kosa na taasisi ama familia ama Biashara lakini zikianzia 20,000 kupanda ama kifungo cha miezi sita.

Pesa hizi zafika zitakiwako zikiwa zoote? Hilo ndilo swali hasa na Je? kama zafika zinatumika katika kazi gani? Maana ninauhakika kuwa hivi ni vyanzo mbadala vya mapato katika manispaa lakini twaenda leo na kuuliza matumizi ya vyanzo hivi vya mapato yakoje nina uhakika hakuna mwenye jibu.

Imeletwa na ndugu AMWESIGA eila lyona ALINDWA.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: