Wasanii wanaotamba katika Muziki wa Kizazi Kipya, Amini na Linah wanatarajia kufufua mahusiano yao upya Machi 17, 2013 ndani ya ukumbi wa Maisha Club jijini Dar es Salaam. Wakizungumza na Kajunason Blog, Amini alisema kuwa ameandaa ma-surprise ya kutosha kwa aliyewahi kuwa mpenzi wake Linah katika kumuonyesha kuwa amerusdi kikamilifu.

Amini aliongeza kuwa siku hiyo mwanadada Linah atakuwa ni siku yake ya kuzaliwa hivyo anazawadi nyingi za kumpa ikiwa ni pamoja na zawadi ya wimbo alioutunga maalum kwa mpenzi wake huyo wa zamani ambaye siku hiyo atatangaza kurudiana nae rasmi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: