Je, mazoezi ya mwili na viungo yana umuhimu gani?

Mazoezi ya mwili ni muhimu kwa binadamu wote, awe mototo au mtu mzima, mnene au mwembamba, mgonjwa au mwenye afya njema. Mazoezi hupunguza uwezo wa kupata saratani, ugonjwa wa kisukari, ugonjwa wa moyo na shinikizo kubwa la damu.
Mazoezi ya mwili pia husaidia kuthibiti magonjwa hayo. Umuhimu mwingine wa mazoezi ya mwili ni kupunguza maumivu ya tumbo wakati wa hedhi, kuzuia ongezeko kubwa la uzito wa mwili, kupunguza msongo wa mawazo na pia kuboresha afyaya akili ikiwa ni pamoja na kuboresha uwezo wa kufikiri, kuelewa (cognitive ability) na kukumbuka.
 Je, nifanye mazoezi ya mwili kiasi gani na aina gani ya mazoezi? 
 
Ili kupunguza uwezekano wa kupata magonjwa sugu yasiyoambukizwa, fanya mazoezi ya mwili angalau kwa dakika 30 kila siku. Yaani, dakika 30 za mazoezi yanayotumia nguvu kiasi kama kutembea kwa haraka (brisk walk) unapoanza unaweza kutumia muda mfupi, na baada ya kuzoea unaweza kuongeza muda hadi dk 0 kwa siku na ukishindwa kabisa kufanya kila siku, fanya angalau dakika 0 mara tatu kwa wiki.
 Namna ya kuongeza mazoezi:
  • Kama unatumia gari, panga shuguli ambazo utafanya kila siku kwa kutembea kwa miguu.
  • Endapo unaishi au kufanya kazi gorofani jitahidi na jizoeshe kutumia ngazi kila siku badala yaq lifti.
  • Unapoenda mahali kwa kutembea tumia njia ndefu badala ya njia ya mkato.
  • Punguza muda unaotumia kutazama televisheni na tumia muda huo kufanya shughuli zinazotumia viungo vya mwili kama kufua, kuosha vyombo, kosha gari, kusafisha nyumba, kazi za bustani na kufyeka majani.
  • Ongeza matumizi ya redio, kwani mara nyingi unaweza kufanya shughuli mbali mbali huku ukisikiliza redio na ikiwezekana uwe na radio ndogo ambayo unaweza kuihamisha na kuiweka mahali unapofanya shughuli zako au mazoezi ya mwili.
  • Watoto wawe na muda wa kucheza kila siku, michezo ambayo inatumia viungo vya mwili kama kukimbia, kucheza mpira, kuruka kamba nk.
Kumbuka, kila zoezi la mwili unalofanya hata kama ni dogo sio sawa na kutofanya kabisa, ni afadhali ufanye kwa kiasi chochote unachoweza kila siku, halafu uongeze polepole.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: