Mafuta
ni muhimu mwilini, isipokuwa yanahitajika kwa kiasi kidogo; hivyo
kuepuka kabisa ulaji wa mafuta huweza kuleta athari katika mwili,
ikiwemo ubongo kutofanya kazi vizuri. Hata hivyo mafuta yanapotumika kwa
kiasi kikubwa yanaweza kuleta madhara mwilini. Hivyo ni muhimu kuwa
makini na kiasi cha mafuta kinacholiwa katika kila mlo.
Kuna aina kuu mbili za mafuta; yale yanayopatikana katika vyakula vya asili ya wanyama nay ale yatokanayo na mimea.
- Mafuta yenye asili ya wanyama
Mafuta
yenye asili ya wanyama huwa yameganda katika joto la kawaida. Mafuta
haya ni kama nyama iliyonona, nyama ya nundu, samli, siagi, jibini na
maziwa yenye mafuta.
Mafuta
haya hayana lehemu kwa kiasi kikubwa. Utumiaji wa mafuta haya huongeza
hatari ya kupata magonjwa ya moyo kuwa na uzito uliozidi na unene
uliokithiri au kisukari. Hivyo ni muhimu kupunguza utumiaji wa mafuta
haya.
- Mafuta yatokanayo na mimea.
Mafuta
yatokanayo na mimea huwa katika hali ya kimiminika katika joto la
kawaida na kwa kawaida haya hayana lehemu. Mafuta haya ni kama mafuta ya
soya, ufuta, karanga, alizeti, mawese, pamba na nazi.
Mifano
mingine ni pamoja na mbegu zitoazo mafuta kama korosho, kweme na mbegu
za maboga. Mafuta haya ndio bora zaidi kuyatumia ukilinganisha na yale
yenye asili ya wanyama kwani huboresha afya ya mwili. Hata hivyo ni
muhimu kuyatumia kwa kiasi kidogo.
Mara nyingi nimesikia lehemu ni mbaya, je ina ubaya gani?
Lehemu
inahitajika mwilini lakini kwa kiasi kidogo. Hata hivyo huwezi kujua
una lehemu kiasi gani mwilini mpk upime (kwa kawaida inatakiwa iwe chini
ya 200mg/dl). Kiasi kikubwa cha lahemu mwilini husababisha mkusanyiko
wa mafuta katika mishipa ya damu na hivyo huweza kuzuia damu kupita kwa
urahisi.
Hali
hii huweza kusababisha shinikizo kubwa la damu na ugonjwa wa moyo.
Hatari nyingine ni mafuta kuziba mishipa midogo ya damu inayoenda kwenye
moyo au ubongo na hivyo kusababisha kiharusi na hata kifo.
Waweza kupunguza hatari hii kwa:
- Kupunguza utumiaji wa nyama, mayai, jibini, na maziwa yasiotolewa mafuta, maini, firigisi, figo. Unapotumia nyama nyekundu isizidi nusu kilo kwa wiki.
- Kuepuka mafuta yatokanayo na wanyama, nyama zilizo nona, ngozi ya siagi na mafuta
- Kuongeza matumizi ya vyakula yenye makapi-mlo kwa wingi kama nafaka zisizokobolewa mfano unga wa dona, ulezi, uwele, mtama vyakula vya jamii ya kunde, mboga mboga na matunda. Kwa kawaida vyakula vyenye makapi-mlo kwa wingi havina mafuta mengi.
- Kufanya mazoezi ya mwili angalau dk 30 kila siku.



Ahsante kwa ujumbe huu!!!
ReplyDelete