

Mbunge
wa Tabora Mjini (CCM) Ismail Aden Rage (wa pili Kulia aliyeshika
bomba) akipambana na vijana wa chadema eneo na mti wa kutundika bendera
za vyama vyao.

Kada
wa Chadema Mkoani Dodoma, Arnold Swai akipokonywa mti wa bendera ya
chadema na wafuasi wa CCM jana, baada ya kutokea vurugu katika eneo la
Mwanga baa, Dodoma

Mmoja
wa Wafuasi wa Chadema akishikwa na polisi baada ya wafuasi wa CCM na
Chadema Kugombea eneo na mti wa kutundika bendera za vyama vyao. Picha
Zote na Mpoki Bukuku
--
SHEREHE
za miaka 36 za kuzaliwa kwa CCM jana ziliingia dosari, baada ya kuibuka
vurugu kubwa kati ya wafuasi wa chama hicho na Chadema mkoani Dodoma
wakati wakigombea eneo na mti wa kutundika bendera za vyama vyao.
Vurugu
hizo zilizotulizwa na Polisi wa Kutuliza Ghasia (FFU), zilitokea jana
mchana katika uwanja huo uliopo karibu na Baa ya Mwanga, baada ya CCM
kung’oa bendera ya Chadema iliyokuwepo uwanjani hapo, ili waweke bendera
zao kwa ajili ya mkutano ambao ulikuwa sehemu ya maadhimisho hayo.
Vurugu
zilizuka baada ya wafuasi wa Chadema kuwataka wenzao wa CCM waendelee
na mkutano katika eneo hilo kwa sharti la kurejeshwa kwa bendera
iliyong’olewa. Wafuasi wa vyama hivyo wakiwamo wabunge wa CCM
walionekana wakivutana kunyang’anyana mti wa bendera.


Toa Maoni Yako:
0 comments: