TANZIA
Mkuu wa Chuo Cha Usimamizi wa Fedha IFM, Anasikitika kutangaza Kifo cha Mwanafunzi Abdul-Aziz Mukasa (pichani) mwenye namba ya usajili BIRM/12/71893 kilichotokea tar. 28.1.2013 kwa kuzama baharini. Mazishi yamefanyika tar 30.1.2013 katika makaburi ya Vijibweni.
Hiyo ndiyo taarifa iliyotoka kwa Mkuu wa Chuo cha IFM kuwapa habari wanafunzi wenzake na marehemu.
Mwanafunzi huyo mauti yalimkuta baada ya mezama na kupotelea baharini
alipokuwa katika Pantoni akivuka akielekea Kigamboni jijini Dar es
Salaam.
TUKIO LENYEWE LILIKUWA HIVI:
Wakizungumza
na Kajunason Blog mashuhuda wa tukio hilo, walisema kuwa mwanafunzi
huyo alikuwa akivuka na wenzake jioni ya leo kuelekea Kigamboni jijini
Dar mara baada ya kutoka kwenye mtihani wake ndipo alipokutwa na mauti
hapo.
Sakata
hilo lilianza mara baada tu ya Pantoni hilo kukaribia eneo la kivuko
cha Kigamboni ndipo mwanafunzi huyo alipoanza kubishano na wanafunzi
wenzake kuwa anauwezo wa kuzamia na kupiga mbizi, katika kuwahakikishia
hilo alivua viatu pamoja na shati lake na kuwapatia wenzake na kujitosa
kwenye maji ili apige mbizi kuwahakikishia wenzake uhodari wake.
"Kiukweli
ni jambo la kushangaza sana, ulitokea ubishani wa wanafunzi baada ya
mwenzetu huyu kuwa anajisifia kuwa anajua kupiga mbizi ndipo alipovua
viatu na shati na kujitosa kwenye maji, kwa bahati mbaya aliangukia
upande wa Pantoni lilipokuwa likipiga makasia na kwa kawaida sehemu hiyo
maji huwa yanakasi sana hivyo yalimsababishia mwanafunzi huyo kushindwa
kuibuka na kumfanya azame katika kina kirefu,"



May his soul R.I.P
ReplyDeleteYou I'll always be in ma heart! Muky RIP. Ameen!
ReplyDeleteBaraka godfrey mkinywa.. Daah inauma kwa kumpoteza mwenzetu ila mimi namuona ni mjinga na nawasii wengine wasifanye upumbavu huu
ReplyDelete