Mkurugenzi Mtendaji Ecobank, Enoch Osei-Safo akiongea na waandishi wa habari katika hafla ya kumzawadia mshindi wa shinda la 'Shinda Babkubwa na Ecobank'
Waandishi wakifuatilia halfa hiyo.
Mkuu wa Domestic Banking, Joyce Malai akiongea na waandishi wa habari machache kabla ya kukabidhi gari kwa mshindi. Pembeni yake ni Mkurugenzi Mtendaji Ecobank, Enoch Osei-Safo pamoja na Mkuu wa Bidhaa na Masoko Ecobank, Andrew Lyimo.
MMM
Gari iliyokabidhiwa mshindi.
Mkurugenzi Mtendaji Ecobank, Enoch Osei-Safo (kushoto) akimkabidhi Mshindi wa Shindano la Babkubwa na Ecobank Bw. Ipyana Mwakasaka gari mpya aina ya Hyundai Tucson ix35.
Mshindi wa Shindano la Babkubwa na Ecobank Bw. Ipyana Mwakasaka akiwa ndani ya gari alilokabidhiwa.
Waandishi wa habari wakifanya mahojiano na Mshindi wa Shindano la Babkubwa na Ecobank Bw. Ipyana Mwakasak.
---
Shindano la Shindano Babkubwa na Ecobank leo lilikamilika kwa makabidhiano ya tuzo kuu ya gari mpya aina ya Hyundai Tucson ix35 kwa mshindi Bw. Ipyana Mwakasaka kutoka Tegeta, Dar es Salaam.
“Nimefurahi sana kuwa mshindi wa tuzo hili la gari jipya zuri ambalo litatusaidia sana mimi na familia yangu katika kutatua shida za usafiri” alisema Bw. Ipyana.
"Ecobank imeonyesha na inazidi kutimiza ahadi yake ya kuridhisha wateja wake pamoja na huduma kwa wateja ya hali ya juu katika matawi yake. Pia mitandao ya Ecobank ya e-banking na ATM zimeturahisishia uendeshaji wa akauti zetu kwa njia iliyo salama zaidi” aliongeza.
Shindano hili lililowalenga wateja binafsi, wanabiashara na kampuni ndogondoga na za kiasi cha kati lilianza Juni 2012 na kuendelea hadi mwisho wa mwaka 2012. Wateja waliokuwa na amana ya 100,000 kuendelea walishiriki kwenya droo hii, ambapo kila mwezi palikuwa na washindi wa iPads, Laptops, vocha zawadi yenye thamani ya shilingi 500,000 na safari kwenda Zanzibar na Ushelisheli " alisema Andrew Lyimo, Mkuu wa Bidhaa na Masoko Ecobank Tanzania.
Hii ni moja kati ya mikakati mingi kwa ajili ya Ecobank kukuza ushirikishwaji wa kifedha kwa Watanzania kwa kutoa huduma nafuu na rahisi ya ufumbuzi wa fedha kwa wanajamii na wafanyabiashara. Lengo letu ni kutoa ufumbuzi wa kifedha ambao umehakikisha mafanikio kwa waAfrika kupitia mtandao wetu mkubwa Afrika nzima, hatua ambayo imedhibitika kukuza ustawi wa kiuchumi "anasema Enoch Osei-Safo, Mkurugenzi Mkuu Ecobank Tanzania.
Ecobank Tanzania ina nia ya kueneza elimu ya kifedha na kuelimisha umma juu ya faida na fursa zilizopo katika sekta ya benki. "Katika miezi michache ijayo, sisi tutazindua mipango ya kukuza zaidi ushirikishwaji wa fedha kwa waTanzania ili kufikia idadi kubwa ya watu ambao hawajafikiwa na huduma za benki" Enoch alielezea. Hii inakwenda sambamba na mkakati wa kitaifa kwa ajili ya kukuza uchumi ili kuwawezesha wananchi kupata faida na fursa katika Tanzania, Afrika na dunia nzima.
Toa Maoni Yako:
0 comments: