Asusa
ni kiasi kidogo cha chakula ambacho sio mlo kamili kinachoweza kuliwa
bila ya matayarisho makubwa. Mara nyingi huliwa kati ya mlo mmoja na
mwingine. Kwa watu wengi hasa wafanyakazi na watoto wa shule ni
vigumu kupata milo yote nyumbani na hivyo inabidi wabebe au wanunue
kiasi kidogo cha chakula hasa cha asubuhi na mchana. Mara nyingi aina
vyakula vinavyopatikana sehemu nyingi ni asusa.
Kwa
bahati mbaya asusa zinazopatikana kwa urahisi katika sehemu za
biashara ni zile zenye mafuta mengi, sukari nyingi na chumvi nyingi
ambazo kiafya sio nzuri. Vilevile mara nyingi mtu anapokuwa na njaa
anakuwa na hamu ya kula chakula chochote bila kuchagua. Hivyo
unashauriwa yafuatayo:
Chagua asusa zenye virutubisho muhimu
Kuwa
mwerevu kwa kuchagua asusa zenye virutubishi muhimu kama matunda,
maziwa, juisi halisi ya matunda, karanga, vyakula vilivyochemshwa au
kuchomwa kama ndizi, magimbi, viazi vikuu, mihogo, mahindi au viazi
vitamu.
Epuka
asusua zifuatazo:
-zilizokaangwa
au kupikwa kwa mafuta mengi kama sambusa, chips, vitumbua, mihogo,
ndizi, na kachori.
-zenye
sukari nyingi kama biscut, visheti, kashata, keki, chokoleti, juisi
bandia, barafu na soda.
Zenye
chumvi nyingi kama krips, bisi zenye chumvi nyingi, soseji nk
Asusa
hizi huweza kuchangia kuongezeka uzito wa mwili na uwezekano wa
kupata kisukari, shinikizo la damu, baadhi ya saratani na magonjwa ya
moyo.
Je
ulishaji wa mtoto una uhusiano gani na magonjwa sugu yasioambukizwa?
Tafiti
zimeonyesha kuwa kuna uhusiano kati ya ulishaji wa mototo na
uwezekano wa kupata magonjwa sugu yasiyoambukizwa utotoni, katika
ujana na hata unapokuwa mtu mzima.
Tafiti
hizo zimeonyesha kuwa kuwa:
- Unyonyeshaji wa maziwa ya mama huwakinga watoto dhidi ya kuwa na uzito uliozidi na unene uliokithiri wanapokuwa wadogo na hapo badae.
- Watoto walionyonyeshwa maziwa ya mama kwa muda mfupi(chini ya miezi sita) na wale waliopewa maziwa mbadala (maziwa ya kopo au ya wanyama) wako katika hatari zaidi ya kupata baadhi ya magonjwa sugu yasiyoambukizwa kama kisukari, shinikizo kubwa la damu na saratani utotoni katika ujana na wanapokuwa watu wazima.
- Ulishaji wa vyakula vya nyongeza vyenye nishati-lishe kwa wingi unahusishwa na motto kuwa na hatari ya kupata unene saratani na shinikizo kubwa la damu ukubwani.
- Unene wakati wa utoto humuweka mtoto katika hatari ya kupata magonjwa sugu yasiyoambukizwa kama kisukari na ugonjwa wa moyo.
Hivyo
mtoto akinyonyeshwa maziwa ya mama pekee kwa miezi sita ya mwanzo na
baada ya miezi sita kupewa chakula cha nyongeza kama inavyoshauriwa
huku mtoto akiendelea kunyonyeshwa maziwa ya mama mpaka anapotimiza
umri wa miaka miwili au zaidi; kuchangia katika kumkinga huyu dhidi
ya magonjwa sugu yasiyo ambukizwa ikiwa ni pamoja na utapiamlo ambao
pia huweza kuleta madhara mengine utotoni na katika utu uzima. Vile
vile, mama anaponyonyesha humpunguzia uwezekano wa kupata saratani ya
matimati.
Je, utumie kwa kiasi gani mboga mboga na matunda? Ungana nasi kesho...
Toa Maoni Yako:
0 comments: