Wazee wa Mtwara wakishangaa kupigwa picha mara baada ya kuwasili nje ya Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo...
Wazee wa Mtwara wakijipanga kuingia katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo...
Wanahabari wakifuatilia mkutano huo.
Katibu wa Wazee wa Mtwara Bw. Seleman Madem ambaye aliongozana na Wazee wa Mtwara kuja jijini Dar es Salaam
kuongea na vyombo vya habari juu ya sakata la gesi. Wazee hao ambao wametoka katika umoja unaoshirikisha vyama mbali mbali vyasiasa ikiwemo ABC,
APP NA MAENDELEO, CHADEMA, DP, NCCR MAGEUZI, SAU, TLP na UDP. Bw. Mademu alisema kuwa wananchi wa Mtwara wanadai kuwa pamoja na yote
hayo kufanyika wao mpaka sasa hawajashirikishwa. Wanamtwara wanasema
kuwa hawakuwa na dhamira mbaya ya kuandamana bali ilikuwa ni kuishinikiza
serikali juu ya sakata la gesi.
Pia waliviasa vyama vya siasa kujichukulia
umaarufu binafsi kwa ajenda ya Gesi, ambao kauli mbiu yao unasema, 'Gesi kwanza
Vyama baadae'. Pia walipinga vyombo vya siasa kuripoti vibaya suala la Mheshimiwa Jemsi Mbatia kuwa hakushushwa jukwaani na wanasema mkutano uliisha kwa amani.
Mwenyekiti wa CHAUMA mkoa wa Mtwara
Bibi Fatuma Selemani ambaye alikuwa ni mmoja ya wazee waliokuja
kuongea na waandishi jijini Dar es Salaam akitilia mkazo suala la
Gesi. Wazee hao walikuja jijini Dar es Salaam kuongea na waandishi wa
Habari ili kuweza kuishinikiza serikali isiisafirishe gesi ya Mtwara
kuja Dar es Salaam.
Jambo ambalo lililoshangaza baada ya Mtandao wa
Kajunason Blog kufanya uchunguzi wake ilibaini kuwa wazee hao
waliletwa na Chama cha NCCR Mageuzi kinachoongozwa na Mh. James Mbatia
kuja jijini Dar es Salaam kumsafisha. Kwa mujibu wa barua
iliyopatikana ndani ya ofisi za ukumbi huo zilionyesha kuwa Ukumbi huo ulikodiwa na Chama hicho jambo lililoonyesha wazi kuwa wazee hao waliletwa na chama hicho japo wenyewe walikataa katu katu kuwa wameuza kuku, mbuzi zao kuja jijini Dar kuzungumzia sakata la gesi jambo ambalo si kweli. Kwa vile mwanzo wazee hao
waliongelea swala la gesi na kupinga kuwa Mh. Mbatia eti hakupigwa
wala kufanyiwa fujo mara baada ya kwenda mjini Mtwara kufanya
mikutano yake ya ndani.
Waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini. Kama ulipitwa na Sakata la Mheshimiwa James Mbatia huko Mtwara... Soma habari hii iliyoandikwa na Gazeti la mwananchi ilikuwa na kichwa cha bari kilichosema, 'Sakata la gesi Mtwara, Mbatia na wabunge wake hatiani' Link hii: http://www.mwananchi.co.tz/habari/Siasa/-/1597332/1664928/-/bop66iz/-/index.html
Toa Maoni Yako:
0 comments: