Katika hali isiyo ya kawaida msanii wa Muziki wa kizazi kipya ambaye pia ni mbunge wa Mbeya Mjini Mh. Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu akiwa ndani ya EATV katika kipindi cha Friday Night Live amemshukia roma na kumuonya kuwa awe mwangalifu na anachokiandika sio kukurupuka na kuandika vitu asivyokuwa na uhakika navyo.

Katika wimbo huo kuna kipande kinasema "Pesa ndio imemaliza bifu ya Ruge na Sugu" Sugu alienda mbali zaidi na kusema madogo wanaokuja juu kimuziki hawamuwezi na ndio maana kawatafutia wa level zao ambaye ni mwanaye Sasha. 

Kwa upande wake Msanii wa Kizazi Kipya Roma ambaye aliandika maneno yeye alikuwa na haya ya kusema.
SITAKI HATA IZUNGUMZWE HII ISSUE LAKINI UNAWEZA UKAPITIA MOJA YA TAFSIRI ZA WIMBO WA 2030 INAWEZA IKASAIDIA
"pesa ilimaliza vita ya ruge na sugu"!!

-shortly ni kuwa issue ya brother sugu kuingia katika vita hii kama ilivyosemwa awali na ilivyoonekana POINT ilikuwa kuitetea sanaa, ambayo ni wasanii pia wakiwemo ndani hapo...kuwa wanachokipata hakistahili kulinganisha na kazi wanayofanya!! malipo mabovu ya show, uuzwaji mbovu wa kazi za sanaa unawafaidisha wengine kuliko wasanii,na mengine mengi sana tuliyasikia!! ambayo kimsingi yote yanaegemea kwenye kipato = pesa!!

Lakini baadae ikaja semwa na pande zote mbili zikakiri kuwa songombingo hilo limeisha baada ya pande zote mbili kukubaliana kuwa yote yaliyokuwa yakilalamikiwa yameeleweka na upande wa brother ruge umekubali kuyamaliza yote yaliyokuwa yakilalamikiwa kuwa sasa yameisha na yanatekelezwa!!

Sasa hiyo ina imply nini? kama yameisha ina maana tatizo la malipo duni ya wasanii, tatizo la wasanii kuingiza pesa nyingi na kulipwa kidogo tofauti na wanachoingiza..na yote yaliyoongelewa SASA YAMEFIKIA KIKOMO!!! BASI NI HABARI NJEMA KWA WASANII.... na hiyo yote ni nini?

- ni kuwa sasa watapata kipato sawa na haki yao!!
-wataifanya sanaa yao kwa njia sahihi na za faida kama ilivyokuwa ikihitajika ktk vita hiyo!!
-na wataiona faida ya sanaa kwa ujumla!!

KIPATO=MALIPO=PESA
BASI PESA NDO IMAMALIZA VITA YA RUGE NA SUGU!!

2030 YA R.O.M.A
NAYAJIBU NINAYOULIZWA NA YANAYOHITAJI UFAFANUZI!!!
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: