Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiweka shada la maua kwenye kaburi la Makamu wa Rais wa Zimbabwe
Marehemu Dkt. Landa John Nkomo wakati wa mazishi yake yaliyofanyika
jana kwenye Makaburi ya Mashujaa jijini Harare.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal
na Mkewe Mama Asha Bilal, wakiwa katika Viwanja vya Makaburi ya Mashujaa
jijini Harare, walipohudhuria maziko ya Makamu wa Rais wa Zimbabwe Marehemu Dkt. Landa John Nkomo yaliyofanyika jana jijini Harare Zimbwabwe.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal
akizungumza jambo na Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe, wakati wakiwa Ikulu
ya nchi hiyo jijini Harare, jana baada ya kumaliza mazungumzo yao. Makamu wa Rais alimtembelea Rais Mugabe kwa lengo la kumfariji kutokana na kifo cha Makamu wake Marehemu Dkt. Landa John Nkomo kilichotokea mwanzoni mwa wiki iliyopita. Dkt. Nkomo alizikwa jana kwenye Makaburi ya Mashujaa jijini Harare Zimbabwe.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal
(kushoto) akizungumza na Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe (kulia)
alipomtembelea Ikulu ya Harare jana kwa lengo la kumfariji kutokana na kifo cha Makamu wa Rais wa nchi hiyo Marehemu Dkt. Landa John Nkoma, kilichotokea mwanzoni mwa wiki iliyopita na kuzikwa jana katika Makaburi ya Mashujaa jijini Harare. Katikati ni Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe Adadi Rajabu.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal
akifurahia jambo na Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe, wakati akiondoka
Ikulu ya nchi hiyo jijini Harare baada ya kumaliza mazungumzo yao. Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais.
Toa Maoni Yako:
0 comments: