Elewa sio kila anayecheka na wewe kafurahi nawe,
Utu wao umo katika "MACHO",
Nafsi zao "ZIMEBEBA"
"Husda"
"Uadui"
"Uchawi"
"Choyo" na
"Roho mbaya".
Furaha zao kukuona "UNAHARIBIKIWA",
Na Hasira zao kukuona "UMEFANIKIWA"
"Ni wangapi!" "uliwaamini!"
"Kuwaheshimu!"
"Kuwapenda!"
"Kuwasaidia!"
"Kuwaona ndugu!"
"Kuwashauri!"
Kuwapa siri? 
Lakini leo ndiyo maadui zako!. Kweli maisha ni watu lakini kuwa Mwangalifu nao. Wamekukuta njiani hawajui ulipo toka, hawajui uliyopitia hata hawajui unakokwenda, Lakini wamejivika umahiri wa kukuchambua na wamegeuka watabiri. Usitumie muda mwingi kuwafikiria, safari yako ni ndefu sana, achana na wapita njia elekeza nguvu zako katika ndoto zako na safari yako katika maisha, tambua mlinzi na kiongozi wako ni MUNGU, sisi wengine mashahidi tu... Nakutakia heri ya Mwaka mpya 2013 wenye mafanikio zaidi. 
MBELE DAIMA, NYUMA MWIKO...

Cathbert Angelo Kajuna,
Founder and Mananging Director
Kajunason Blog.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: