Mgambo wa jiji la Dar es Salaam akitekeleza majukumu yake leo, ya kulifunga mnyororo gari lenye namba za usajili T 569 BHD lililokuwa limepaki vibaya pembeni mwa barabara maeneo ya feli jijini Dar es Salaam.
Akijiweka sawa mara baada ya kumaliza kufunga.
 Huyu dereva aliamua kulipaki gari lake kwa staili hii na kuamua kuondoka bila kutoa maagizo yeyote.
Baada ya kuwa amelifunga mgambo huyo wa jiji la Dar akichukua kalamu yake na kuanza kuandika dondoo muhimu. Mgambo huyo baada ya mtandao huu kunyaka akifanya tukio hili, Ulifanya nae mahojiano nae machache juu ya kazi hiyo aliyofanya na alisema kuwa wanapomaliza kufunga huwa wanamsubiri mwenye gari mpaka anapokuja na kuandikiwa faini ya Tsh. 80,000/- kwa kitendo chake cha kupaki sehemu isiyorasmi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: