Meneja wa kinywaji cha Castle Lite Pamela Kikuli akimpongeza mshindi wa shindano la 'Feel the Beet of Sub Zero' nchini Afrika Kusini, Caroline Lupilli lililoendeshwa kwa kuwashirikisha washiriki wa mtandao wa facebook.
Meneja wa kinywaji cha Castle Lite Pamela Kikuli akimpongeza mshindi wa shindano la 'Feel the Beet of Sub Zero' nchini Afrika Kusini, Caroline Lupilli lililoendeshwa kwa kuwashirikisha washiriki wa mtandao wa facebook.
---
Na Mwandishi Wetu
WATANZANIA watatu waliobahatika kuhudhuria tamasha kubwa la muziki lijulikanalo kama ‘Feel the Beet of Sub Zero’ wamejulikana.
Tamasha hilo la kimataifa linaloandaliwa na kinywaji cha Castle Lite, linatarajiwa kufanyika Johannesburg, Afrika Kusini Februari 2, mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Meneja wa Bia ya Castle Lite inayozalishwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Pamela Kikuli, alisema watu hao watalipiwa kila kitu ikiwa pamoja na nauli ya kwenda na wenza wao watakaowachagua.
Pamela aliwataja watu hao ambao walipatikana kupitia shindano lilikuwa likiendeshwa katika kurasa ya Castle Lite kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook, kuwa ni Caroline, Edger na Eric.
“Hii ina maana kuwa Castle Lite itawalipia watu sita ikiwa ni gharama za kwenda huko, kwani tulisema kila mmoja ataenda na rafiki yake atakayemchagua. “Tumefanya hivi ikiwa ni kurudisha fadhila kwa jamii, maana kwa kiasi kikubwa imetuunga mkono katika mambo mbalimbali,” alisema.
Mwanamuziki maarufu atakayetumbuiza katika tamasha hilo ni Kanye West.
Toa Maoni Yako:
0 comments: