Mkurugenzi na muasisi wa kituo cha kulelea watoto yatima, kinachoitwa Malaika Orphanage Foundation, Rahma Manji (Pichani kushoto) alipokea msaada kutoka kwa mwambata wa Jeshi kutoka nchini Ujerumani, Bw Abel Gunta(Pichani kulia) ambaye aliguswa na moyo wa mwenyekiti huyo aliyemua kuanzisha kituo cha kusaidia watoto baada ya yeye mwenyewe kujikuta akilea watoto wengi wa ndugu zake kwa sababu mbali mbali takriban miaka 1o iliyopita.
Gunta pia alikabidhi fulana ambazo zitatumika kama sare baada ya masomo kwa watoto hao, hapa akishiriki katika kuwakabidhi watoto wenyewe. Kituo hicho kilichopo Mkuranga, Mkoa wa Pwani kina watoto 61 wanaoishi hapo huku 48 wakiwa wanasoma za msingi zilizopo wilayani Mkuranga, saba shule ya Sekondari na waliobaki wakiwa hawajafikia umri wa kwenda shule
Picha ya pamoja ya wanakituo.
---
---
Kituo kinakabiliana na changamoto mbali mbali katika kipindi hiki ambacho bado hawana miradi ya kujiendesha, vitu kama mavazi, chakula, ada za watoto ambao wanasoma nje ya Kituo, na waalimu wa kujitolea kuwafundisha watoto masomo ya ziada baada ya saa za masomo. Kufuatia hilo ndugu mdau unakaribishwa kutembelea Kituo na kujionea hali halisi na kutoa chochote. Kwa maeleozo zaidi unaweza kupiga namba +255 655 786 011 ama unaweza kutuma mchango wako kwa kituo kupitia akaunti ya KBC namba 3300828357.
Toa Maoni Yako:
0 comments: