• Wateja wawili wa Airtel kujinyakulia kitita cha shilingi milioni 15
• Promosheni ya amka millionea bado inaendelea
Kampuni ya simu za mkononi Airtel bado inaendelea kuwazawadia wateja wake kupitia promosheni ya Amka Millionea ambapo imetangaza kuchezesha droo ya pili ya mwisho wa mwezi kesho jumanne tarehe 29 itakayowawezesha wateja wake wawili kuibuka na kitita cha shilingi million 15 kila mmoja
Akizungumza juu ya droo hiyo Meneja Uhusiano wa Airtel bwn Jackson Mmbando alisema, “tangu ilipozinduliwa mwanzoni mwa mwenzi December mwaka jana tumekuwa tukiwazawadia wateja zawadi za pesa taslimu kila siku, kila wiki na kila mwenzi. Droo ya kwanza ya mwenzi wa December ilifanyika na kushuhudia Agnes Hassani Chakame mwenye umri wa miaka 27, mkulima na makazi wa Rufiji pamoja na Rickson Richard Kilonzo mwanafunzi wa kidato cha 5, umri wa miaka 19 ambae ni mkazi wa Arusha wakiibuka mamilionea kila mmoja akiondoka kitita cha shilingi milioni 15”.
“Na leo tunayofuraha kuwatangazia droo ya mwenzi Januari ambapo wewe pia una nafasi ya kuibuka kuwa mshindi, droo hii itafanyika kesho saa tano hapa makao makuu ya Airtel Moroco na washindi kutangazwa mara baaada ya droo hiyo Ikiwa hujashiriki unaweza kujaribu bahati yako sasa!
Ili mteja aweze kushiriki inabidi atume neno WIN/SHINDA kwenda namba
15595 bure , Baada kujiunga mteja atapata ujumbe kutoka 15656 na kupata maswali ambayo atajibu na akipata sahihi atapata ponti 20 akikosea atapata ponti 10. Na kwakila ujumbe atakaotuma atatozwa kiasi cha shilingi 350 pamoja na kodi.
Airtel tunaahidi kuendelea kuboresha huduma zetu na kuendelea kuwazawadia wateja wetu kupitia promosheni mbalimbali huku tukiwapatia huduma nafuu kupitia mtandao ulioenea zaidi nchini. Aliongeza Mmbando
Mbali na promosheni hii kabambe, Airtel pia imekuwa mstari wa mbele kutoa gharama nafuu za mawasiliano kwa wateja wote nchini, Airtel imeimepunguza gharama za kutuma sms, ujumbe mfupi pamoja na gharama za kupiga simu ambapo kwa sasa mteja wa Airtel atatozwa shilingi 1 kwa sms moja siku nzima mara baada ya kutuma ujumbe mfupi wa kwanza kwa shilingi 125, na pia gharama za kupiga simu kwenda Airtel kwa Airtel sasa ni senti 10 mara baada ya dakika mbili za kwanza.
Toa Maoni Yako:
0 comments: