BALOZI wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China, Lu Youqing, amemkabidhi Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo, Fenella Mukangara, vifaa vya michezo vyenye thamani ya dola za Kimarekani 50 (sawa na Sh milioni 80), ili kuendeleza utamaduni wa Tanzania.

Akikabidhi vifaa hivyo jijini Dar es Salaam Balozi Youqing, alisema Tanzania ni nchi ambayo ina ushirikiano wa karibu na Serikali ya watu wa China, hivyo katika kuendeleza utamaduni wa Tanzania, wameamua kutoa vifaa hivi vya michezo vitakavyoweza kuinua utamaduni wa nchi hiyo.

Alisema Juni mwaka huu nchi 46 ikiwemo China na Afrika, ziliwakilisha tamaduni zao katika mjini Beijing, ikiwa na lengo la kuweza kujifunza tamaduni za nchi mbalimbali ikiwemo Afrika ila tulifurahishwa na utamaduni wa Tanzania.

Waziri Mukangara akizungumza baada ya kupkea vifaa hivyo, alisema utamaduni ndio utambaulisho wa kila mtu ambao unamsaidia katika jamii au nchi katika kumtofautisha na mtu mwengine.

“Vifaa hivi nitavikabidhi katika Chuo cha Sanaa Bagamoyo (TASUBA), ambavyo vitatumika kwa ajili ya kuutangaza utamaduni wa nchi yetu,” alisema.

Alisema chuo cha Tasuba kilianzishwa kwa lengo la kufundisha umuhimu wa utamaduni wa nchi yetu, kwani sekta ya utamaduni ndio mwanvuli wa kila kitu ikiwa ni pamoja na lugha, sanaa, kabila pamoja na uchoraji, vifaa vilivyotolewa ni pamoja na Gitaa, Ngoma na vifaaa mbalimbali vya kuendeleza shughuli za muziki.

Alisema Serikali ya jamhuri ya watu wa China imekuwa mstari wa mbele katika kuisaidia nchi ya Tanzania hususani katika suala zima la kuendeleza utamaduni wa nchi ya Tanzania.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: