Mwanamuziki  Kofii Olomide akiimba jukwaani na kundi lake katika Onesho  linalofanyiki usiku huu  kwenye viwanja vya Leaders Kinondoni jijini Dar es salaam ambapo wageni waalikwa na mashabiki mbalimbali wamefurika katika viwanja hivvyo , ili waweze kushuhudia shughuli pevu ya mwanamuziki huyo nguli wa muziki  Barani Afrika.
Fullshangweblog na kikozi kazi chake chote iko katika eneo la tukio ili kukumuvuzishia matukio  yatakayojiri katika viwanja vya Leaders usiku huu moja kwa moja katika kukupasha habari na kukuburudisha pia.
 
Mmoja wa wanenguaji wa mwanamuziki Kofii Olomide akifanya vitu vyake jukwaani kama anavyoonekana katika picha.
Kofii Olomide akiimba na mmoja wa waimbaji wake Cindy.Mwanamuziki Kofii Olomide  akiwa na mmoja wa waimbaji wake wa kike wakipagawisha mashabiki wa bendi hiyo  waliojitokeza kwa wingi katika viwanja vya Leaders ili kushuhudia kile anachokifanya jukwaani.
Wanamuziki wa Skylight Band wakikamua.
First Lady wa Mwanamuziki Kofii Olomide, Mama Cindy akikamua.
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Clouds Media Group akizungumza kumshukuru mwanamuziki Kofii Olomide na mashabiki waliojitokeza kwa wingi katika onesho hilo kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam.
                 
Viongozi wa Mapacha Watatu
Wacheza show wa Mwanamuziki Koffi Olomide.
Wanamuziki wa Bendi ya Diamond Sound.
Vimwana wanenguaji wa mwanamuziki Kofii Olomide wakimwaga mauno kwa kwenda mbele jukwaani katika onesho hilo.
Mwanamuziki Kofii Olomide akiwa amezungukwa na vimwana hao ambao ni wanenguajia wa bendi yake huku akiwa katikati yao kama mfalme.
 
Hapa ni Burudani ya mauno tu kama inavyoonekana madau.
Mashabiki mbalimbali wa mwanamuziki Kofii Olomide wakifuatilia kwa makini wakati mwanamuziki Kofii Olomide akiimba jukwaani.
Mashabiki wa mwanamziki Kofii Olomide wakishangilia kwa furaha wakati mwanamuziki Kofii Olomide akiimba jukwaani.
Mwanamuziki Kofii Olomide akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Kampuni ya bia ya Serengeti Bw. Steve Gannon wa pili kutoka kushoto na Mkurugenzi wa Masoko Bw. Ephraim Mafuru pamoja na wafanyakazi wengine.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: