Mkurugenzi wa Kampuni ya Rena Event Limited Bw Rena Calist akizungumza na waandishi wa habari kwenye hoteli ya Sea Escape iliyoko Mbezi Afrikana jijini Dar es salaam wakati akizungumzia matayarisho ya mwisho kabla ya shindano la Miss East Africa linalotarajiwa kufanyika kesho Desema 21 kwenye ukumbi wa Mlimani City Dar es salaam.
Katika shindano hilo wanashiriki warembo kutoka mataifa mbalimbali ya ukanda wa nchi za Afrika Mashariki na na baadhi ya nchi jirani na ukanda h ambapo mshindi wa shindano hilo anatarajiwa kujinyakulia zawadi zenye thamani ya dola za Kimarekani elfu thelathini 30,000.
Kushoto ni Guetano Kagwa ambaye atakuwa MC wa shindano hilo na kulia ni Serge Nkurunzinza Mwakilishi wa Miss East Africa nchini Burundi .
Guetano Kagwa ambaye ni MCwa shindano hilo akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano huo uliofanyika leo jijini Dar es salaam, kulia ni Rena Calist Mkurugenzi wa Miss East Africa.
Warembo wanaoshiriki katika shindano hilo wakiwa katika mkutano na waandishi wa habari leo.
 
Warembo wanaoshiriki katika shindano hilo wakiwa katika mkutano na waandishi wa habari leo.
Warembo wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa mkutano na waandishi wa habari leo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: