Makamu wa Rais Dk. Mohammed Galib Bilal, akisaini katika kitabu cha
maombolezo ya kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Tabora mjini,Siraju
Kaboyonga, aliyefariki dunia juzi na kuzikwa jana jijini Dar es Salaam.
Makamu alifika kuhani msiba huo nyumbani kwa marehemu Sinza jijini Dar
es Salaam jana.Katikati ni Balozi Mstaafu, Hashim Mbita na Mwenyekiti wa
Chama cha Cuf, Prof.Ibrahim Lipumba.Picha na OMR
Makamu wa Rais akiagana na waombolezaji wakati akiondoka eneo hilo.
Toa Maoni Yako:
0 comments: