
Leo
Jumamosi Dec 29 ni mwaka mmoja tokea mtangazaji wa kwanza wa kike
kutangaza mpira katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na kati Halima
Mchuka (pichani) kufariki dunia.
Halima
Mchuka atakumbukwa kwa weledi wake wa hali ya juu katika tasnia ya
utangazaji, hasa wa mpira ambapo aliweza kubuni maneno na majina mengi
ambayo yanatumika hadi hii leo, mfano mkubwa ni 'mpira umeenda fyongo'
akimaanisha mpira umepigwa vibaya na mchezaji.
Leo
saa kumi jioni kutakuwa na kisomo nyumbani kwa dada yake Mwajuma
Mchuka Mbezi Beach, Dar es salaam. Karibuni wote kumuenzi na kumuombea
dua shujaa huyu.


Toa Maoni Yako:
0 comments: