Mkurugenzi wa Kampuni ya Glitz Entertainment Limited, ambao ni waandaaji wa tamasha la TOTO PARTY, Bw. Dennis Ssebo akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari juu ya tamasha hilo la watoto linalotarajia kufanyika tarehe 25 na 26 Desemba 2012 katika ufukwe wa Cine Club jijini Dar es Salaam. Pembeni ni Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa na Masoko ya ECO Bank Bw. Andrew Lyimo.
Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa na Masoko ya ECO Bank Bw. Andrew Lyimo (wa kwanza kulia) akiongea kuelezea jinsi benki hiyo ilivyojitoa kudhamini tamasha la TOTO PARTY. Pembeni yake ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Glitz Entertainment Limited, ambao ni waandaaji wa tamasha la TOTO PARTY, Bw. Dennis Ssebo na Meneja wa Masuala ya Biashara Bw. Adenkule Adewaye.
Meneja wa Masuala ya Biashara Bw. Adenkule Adewaye (wa kwanza kushoto) akielezea machache yanayohusu benki yao.
---
Na Mwandishi Wetu
KATIKA kuhakikisha watoto nao wanapata nafasi ya kusheherekea vema sikukuu ya Krismasi vema, kampuni ya Giltz Limited ya jijini Dar es Salaam imeandaa tamasha maalumu kwa ajili kuwaburudisha maarufu kama “Toto Party”.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Glitz Entertainment Limited Bw. Dennis Ssebo alisema tamsaha hilo la Toto Party itafanyika katika ufukwe wa Cine Club uliopo Mikocheni ikiwa ni safari ni mara ya tatu mfululizo kufanywa kwa watoto wa Dar es Salaam.
“ Hii itakuwa ni mara yetu ya tatu kuandaa sherehe hizi kwa ajili ya watoto hapa Dar es Salaam na kwa mara ya kwanza itafanyika mara mbili tofauti na ilivyokuwa imezoeleka kwani sasa itafanyika Krismasi na Boxing Day hapo hapo Cine Club,” alisema Ssebo.
Katika sherehe hizo mbili watoto watapata nafasi ya kushiriki katika michezo mbalimbali kama soka la ufukweni, kuogelea, kusaka hazina (Treasure hunt) na kujipaka rangi usoni (Face painting) na mengine mengi.
Aidha watoto hao pia wataweza kufunga akaunti ya benki kwa watoto inayojulikana kama ‘Pambazuka’ kupitia benki ya Ecobank.
Mbali na watoto kucheza na kufurahi michezo mbalimbali pia wazazi wao watachuana katika mchezo wa kuvuta kamba ambapo washindi katika michezo hiyo watazawadiwa zawadi mbalimbali na viingilio ni Sh 3,000 kwa watoto na wakubwa Sh 7,000.
Waratibu wa sherehe pia wamebainisha kuwa mwakani mbali na Dar es Salaam, sherehe hizo pia zitafanyika kwenye katika mikoa ya Arusha na Tanga.
Toa Maoni Yako:
0 comments: