Na Heka Wanna na Shakila Galus, MAELEZO

MWENYEKITI wa WAMA Mama Salma Kikwete (pichani) ametoa wito kwa wananchi wenye tabia ya kujisomea vitabu na machapisho mbalimbali ili kujiongezea maarifa yatakayowawezesha kujiletea maendeleo.

Mama Kikwete alitoa kauli hiyo kwenye Makumbusho ya Taifa jana jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa makataba kwa ajili ya watoto na watu wazima.

Alisema kuwa elimu ndiyo silaha pekee ya kukabiliana na maadui watu ambao ni ujinga, maradhi na umaskini na hivyo kujiletea maendeleo.

Mama Kikwete aliongezea mbinu za kujiendeleza kimaisha zinapatikana pia kwa njia elimu kupitia vitabu na machapisho mbalimbali yanayopatikana kwenye maktaba mbalimbali ndani na nje ya Tanzania.

Alisema kuwa hiyo itasaidia katika kuongeza maarifa kwani kutakuwa na vitabu, kompyuta na mitambo ya mawasiliano ambayo itawawezesha watumiaji kupata elimu ya taaluma mbalimbali.

Aidha Mama Kikwete aliwasihi watumishi wa Makumbusho hiyo kuwa ni jukumu lao kutunza maktaba hiyo ili isaidie kukidhi malengo ya kuanzishwa kwake kwa kuandaa taratibu bora za kudhibiti matumizi yasiyo na tija ya maktaba ikiwemo upotevu machapisho na vitabu mbalimbali na uhalibifu wa vitabu unaofanywa na watu wasiotaka maendeleo.

Mwenyekiti huyo WAMA alimshukru Balozi wa Korea Kusini Young Shimo Dho kwa niaba ya nchi yake kwa msaada wa vitabu na vifaa mbalimbali kwa ajili ya maktaba hizo mbili.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: