NA SURAH MATANDA, DAR

BENKI YA DUNIA IMETOA THAMANI YA BILIONI 300 KWA AJILI YA KUANDAA MPANGO KABAMBE WA MAZINGIRA NA BIASHARA (MASTER PLAN) KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM AMBAO UTAWEZA KUFANIKISHA KUTENGENEZA NA KUPANUA JIJI KWA MIAKA ISHIRINI IJAYO.

HAYO ALIYASEMWA KWENYE MKUTANO WA SIKU TATU WA WADAU MBALIMBALI WA MPANGO WA JIJI AMBAO WANAWASILISHA MAONI YAO YA AWALI NA KUFANYIWA MAREKEBISHO YA MWISHO KWANI YAMEPITWA NA WAKATI.

AKIELEZA JUU YA SUALA LA MPANGIO MIJI KATIKA SUALA LA MAZINGIRA MHANDISI MKUU WA JIJI BW MARTIN NATI AMESEMA KUWA MASTER PLAN ILIYOKUWEPO MWAKA 1979 IMECHANGIA KIASI KIKUBWA KURUDISHA NYUMA MAENDELEO YA JIJI KUTOKANA KUTOBADILISHWA KWA MUDA MREFU.

NAYE AFISA MIPANGO MIJI MKUU WA DAR ES SALAAM BW TOMMY KAPINGA ALIONGEZA KUWA UKOSEFU WA FEDHA NA MPANGO MADHUBUTI WA JIJI UMESABABISHA MJI KUKOSA MIUNDOMBINU THABITI, UJENZI HOLELA NA JIJI KUPOTEZA DIRA.

MASTER PLAN ITAKAYOKUBALIWA ITAKUWA NA MPANGO WA JIJI KWA KIPINDI CHA MWAKA 2012-2032.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: