Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif
Sharif Hamad akizindua Ripoti ya Idadi ya Watu Duniani kwa mwaka 2012, huko
Mkwajuni Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif
Sharif Hamad akionnyesha Ripoti ya Idadi ya Watu Duniani kwa mwaka 2012, baada
ya kuizindua rasmi huko Mkwajuni Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanziba Maalim Seif
Sharif Hamad akizungumza na MWakilishi Mkaazi wa UNFPA Tanzania Mariam Khan baada
ya kuzindua Ripoti ya Idadi ya Watu Duniani kwa mwaka 2012, huko Mkwajuni Mkoa
wa Kaskazini Unguja.
Waziri wa Afya Juma Duni Haji akiungana na kikundi
cha Sanaa Zanzibar kutoa burudani ya ngoma ya Msewe wakati wa uzinduzi wa Ripoti
ya Idadi ya Watu Duniani kwa mwaka 2012, huko Mkwajuni Mkoa wa Kaskazini
Unguja.
---
Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi zanzibar
Idadi ya vifo vya akina mama wajawazito
imepungua kwa kiasi kikubwa hapa nchini katika miaka ya hivi karibuni
ikilinganishwa na miaka ya nyuma.
Hayo
yamebainishwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif
Sharif Hamad wakati akizindua Ripori ya Idadi ya Watu Duniani ya mwaka
2012 iliyofanyika Mkwajuni Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Katika hafla hiyo, Maalim Seif alikuwa akimwakilisha Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohd Shein.
Amesema
ingawa vifo vitokanavyo na uzazi duniani bado ni tishio, laikini kwa
upande wa Tanzania idahio hiyo imepungua kutoka vifo vya akina mama 578
katika mwaka 2004 na 2005 na kufikia vifo vya watu 473 mwaka 2006 hadi
vifo 281 mwaka 2011, kwa kila mama wajawazito 100,000.
Hata hivyo, Maalim Seif amesema kuwa vifo hivyo viko juu katika mataifa mbalimbali duniani.
Akizungumzia
kwa upande wa Zanzibar, Makam huyo wa Rais amesema vifo vya akina mama
vitokanavyo na uzazi usio salama vimepungua kutoka watu 473 kwa mwaka
2006 hadi kufikia vifo vya watu 281 kwa mwaka 2011, kwa kila akina mama
100,000.
kutokana
na hali hiyo, Maalim Seif amesema ipo haja ya jamii kuelimishwa zaidi
juu ya umuhimu wa uzazi salama na kupunguza vifo vya watoto na
kuimarisha mpango kwa maendeleo ya taifa letu.
Hata
hivyo amesema jamii bado haijatoa umuhimu unaostahili katika matumizi
ya njia za uzazi wa mpango salama hali inayopelekea kuwepo kwa ongezeko
kubwa la watu.
“Taarifa
zinaonesha kwamba Zanzibar hivi sasa inakadiriwa kuwa na idadi ya watu
1.3 milioni, wanaoongezeka kwa kasi ya asilimia 3.1 kwa mwaka ambapo
idadi ya watu katika kila kilomita moja ya mraba imefikia watu 496 mwaka
2011”, ilieleza sehemu ya hotuba hiyo ya Dkt. Shein iliyosomwa na
Makamu wa Kwanza wa Rais.
Amesema
kupungua kwa vifo hapa nchini kunatokana na juhudi za serikali katika
kuimarisha huduma za afya na utoaji wa chanjo kwa akina mama na ikiwemo
ya pepopunda na surua kwa mtoto wachanga.
Kwa
upande wao wawakilishi wa Umoja wa Mataifa wameipongeza Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuona umuhimu wa huduma ya uzazi na kuamua
kutoa huduma hiyo bila ya malipo.
Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la Idadi ya watu (UNFPA) Tanzania bibi Mariam Khan
amesema bado suala la uzazi wa mpango linakabiliwa na changamoto nyingi
ikiwa ni pamoja na wanajamii kuona ugumu juu ya matumizi ya njia za
uzazi wa mpango.
Amefahamisha
kuwa uzazi wa mpango ni muhimu katika kusaidia kukuza kipato cha
wanafamilia, sambamba na kuwaendeleza watoto katika makuzi bora, na wito
kwa jamii kutoa fursa zinazostahiki kwa akina mama na watoto ili
kusaidia harakati za maendeleo kwa jamii.
Naye
Waziri wa Afya wa Zanzibar Mh. Juma Duni Haji, amesema wizara yake
itaendelea na mpango wa utoaji elimu kwa jamii ili kuongreza uelewa
zaidi kwa wananchi wa Visiwa vya unguja na Pemba.
Amesema
akinamama na watoto wanahitaji kulindwa kiafya, na kuwataka wazazi
kushirikiana katika suala la malezi na makuzi ya watoto.
Mapema
akitoa muhtasari wa ripoti hiyo, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Uchumi na
Mipango ya Maendeleo Khamis Mussa Omari, amesema zaidi ya wananwake
milioni 222 duniani kote hawapati huduma bora za mpango wa uzazi salama.
Amesema
amkina mama zaidi ya milioni 80 hupata mimba zisizotarajiwa na kati ya
hao akina mama 40 milioni hutoa mimba na hata kuhatarisha maisha ya
viumbe vilivyopo tumboni na mama husika.
“Inakisiwa
kuwa kiasi cha mimba milioni 80 zinapatikana bila ya kutarajiwa
duniani, huku nusu ya mimba hizo zikitolewa, jambo ambalo ni hatari
nyengine katika uzazi”. Alidokeza Katibu Mkuu huyo.
Amesema
uzazi wa mpango ni miongoni kwa haki za binadamu lakini imeelekezwa
zaidi kwenye haki za kifamilia, ili wanafamilia waweze kupanga juu ya
idadi na umri wa kupishana kwa watoto, ili kuepuka mimba zisizotarajiwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments: