Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (NEC) kimekutana katika Ukumbi wa mikutano wa Makao Makuu ya chama, maarufu kama Whitehouse mjini Dodoma,leo tarehe 14th Nov 2012.
Kikao hicho kitajadili juu ya kuunda na kupitisha majina
yaliyopendekezwa na Mwenyekiti wa Chama Mapinduzi Mheshimiwa Dkt Jakaya
Mrisho Kikwete, ya wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama ya Taifa (CC) pamoja
na uundaji wa sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa.
Mwenyekiti
wa Chama kwa mujibu wa Kanuni na Katiba ya Chama Cha Mapinduzi, anayo
fursa ya kuteua wajumbe kumi(10) wa Halmashauri kuu ya Taifa, ambapo
Mwenyekiti aliwateua wajumbe wanne(4) na akabakiza nafasi nyingine sita
(6) miongoni mwa wajumbe hao ni Mhe. Asha-rose Migiro, Mhe. Zakhia
Meghji, Mhe. Nape nnauye na Mhe. Abdulrahaman Kinana .
Baada ya uteuzi huo Mwenyekiti pia alipendekeza majina ya Wajumbe wa
Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa, ambapo alipendekeza majina
yafuatayo;
- Nafasi ya Katibu Mkuu, alimpendekeza Mhe. Abdulrahaman kinana.
- Nafasi ya Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Mhe. Vuai Ali Vuai.
- Nafasi ya Naibu Katibu Mkuu Bara, Mhe. Lameck Madelu Nchemba.
- Katibu wa Oganaizesheni ni Ndugu Mohamed Seif Khatibu.
- Katibu wa Siasa na Mahusiano ya Kimataifa, Asha-rose Migiro.
- Katibu wa Uchumi na Fedha, Zakhia A. Meghji.
Baada ya mapendekezo hayo, Halmashauri Kuu ya Taifa ilipitisha majina
hayo na kuyakubali kuwa hao waliopendekezwa ndio hasa wanaofaa kuwa
wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa.
Pia, Mwenyekiti akawashukuru wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa
waliopita na pia kuwataka wajumbe wapya kuchapa kazi, na kuwataka
kujenga mustakabali wa Chama, Uimara na Umadhubuti kwa kufanya kazi kwa
kushirikiana na kusaidiana.
Abdulrahman Kinana-Katibu Mkuu wa CCM, Taifa
Mwigulu Nchemba-Naibu Katibu Mkuu (Bara)
Vuai Ali Vuai-Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar)
Nape Nnauye-Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi
Asha-Rose Migiro- Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa
Zakia Meghji-Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha
Muhamed Seif Khatib, Katibu wa NEC, Oganaizesheni
Toa Maoni Yako:
0 comments: